RC KATAVI: KILA MMOJA ACHUNGE MKE WAKE NA MUME WAKE.


Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumza na waadishi wa habari leo mapema ofisini kwake.

Na George Mwigulu,Katavi.

Wananchi wa Mkoa wa Katavi wameombwa kutokujihusisha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na kusababisha vifo ambapo kitendo hicho ni kinyume na sheria za nchi ambazo zinalida uhai wa mtu.

Wananchi wa Mkoa wa Katavi wameombwa kutokujihusisha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na kusababisha vifo ambapo kitendo hicho ni kinyume na sheria za nchi ambazo zinalida uhai wa mtu.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko amesema hayo jana ofisini kwake alipokuwa akizungumza na wanahabari juu ya maadalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kupokelewa Septemba,23 Mwaka huu katika Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mrindoko amesema kuwa kupitia chunguzi zilizokwisha kufanyika mkoani hapo ni kuwa matukio mengi ambayo wamekuwa wakiyapokelewa ni yale yanayotokana na migogoro ya wivu wa mapenzi,imani za kishirikiana na migogoro ya kifamilia ambayo imekuwa ikisababisha vifo vya watu wa ndani au nje ya familia.

Mkuu wa mkoa huyo amekili bado kuwepo kwa matukio hayo lakini yamepungua ambapo alitoa wito kwa jamii kuwa ni marufuku na hairuhusiwi kujichukulia sheria mkononi na endapo migogoro yoyote ya ardhi au ya kifamilia inatokea yupo mwenyekiti wa kijiji,mabaraza ya vijiji kata,wilaya,Mahakama na hata ofisi za serikali ambazo ni sehemu ya kutatua migogoro hiyo kiutawala.

Vilevile wananchi wa Mkoa wa Katavi kurejea kwenye maadili na kuendelea kuzingatia mafundisho ya dini,kwani kwa kuzingatia mafundisho hayo hakuna mtu atakayeweza kujichukulia sheria mkononi ikiwa pamoja kuepuka vitendo vya kinyume na maadili kama vile ubakaji,ulawiti na kupigana na kujeruhiana na kutoa uhai.

Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa huyo ameiomba jamii kujitahidi kuwafundisha watoto maadili mema,Na kufuatilia mwenendo wa watoto hasa vijana ambao wanaendelea kukua kwa sababu wakati mwingine vijana hao wanafanya matukio kupitia vikundi vya kiharifu.

" kila mazazi achunge mtoto wake,achunge mke na mume wake,achunge ndugu zake na achunge kila mwanafamilia ili kuhakikisha kwamba wote hao hawajihusishi na vitendo vya kiharifu...lakini pia hakuna ambaye anakiuka maadili yanayosababisha watu kujeruhiana na kutoleana uhai" Alisema Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko.

Aidha Mrindoko amesema kuwa serikali ya Mkoa wa Katavi imepiga hatua kubwa ya kudhibiti kikundi cha vijana waharifu wanaofahamika kwa jina la (Damu Chafu) waliokuwa wakivunja nyumba,kupora mali,kupiga na kujeruhi mwili.

Baadhi ya Wanahabari wa Mkoa wa Katavi wakiendelea na majukumu yao ya kikazi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Hivyo amewaomba wananchi endapo wataona dalili za vikundi vyovyote watu hasa vijana wanaowahisi kupanga kufanya uhalifu watoe taarifa haraka ili serikali waendelee kuchukua hatua kali zaidi.

Paul Mathias,Mkazi wa Mtaa wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda aliishukuru serikali kupitia jeshi la Polisi kufanya kazi kubwa ya kuwadhibiti vikundi vya uharifu  hasa Damu Chafu ambao walikuwa wakihatarisha maisha ya watu.

Mkazi huyo wa Makanyagio amesema kuwa kwa sasa wanauhuru wa kufanyabiashara bila mashaka yoyote yale,na hali ya utulivu katika mkoa huo utachochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

Happy Nkondola,Mkazi  wa Mtaa wa Shanwe Manispaa ya Mpanda amesema kuwa kudi la Damu Chafu lilikuwa ni hatari hasa kwa wanawake wajasiriamali kwani wanawake wengi wameporwa mali zao.

Licha ya juhudi kubwa kufanywa ya kudhibiti kundi hilo,ameiomba serikali kupitia Jeshi la Polisi kuendelea kuimarisha ulizi zaidi wa watu na mali zao.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages