KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ADUWAA UBORA WA MIRADI MLELE.

Majengo ya madarasa ya shule ya sekondari Kamsisi iliyowekewa mawe ya msingi na mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2022.

Na Walter Mguluchuma,Mlele.

Kukamilika kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kamsisi imeelezwa kuwa itakuwa mkombozi kwa wanafunzi wanaotembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa nane hadi kumi na tano kila siku kufuata masomo shule  ya jirani ya Inyonga iliyoko Kata ya Inyonga.

Madaraka ya shule ya sekondari Kamsisi yaliuojengwa kwa fedha za SEQUIP ambayo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2022,Sahili Geraruma ameyasifia ujenzi wake kuwa niya ubora unaohitajika.

Kukamilika kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kamsisi imeelezwa kuwa itakuwa mkombozi kwa wanafunzi wanaotembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa nane hadi kumi na tano kila siku kufuata masomo katika shule  ya jirani ya Inyonga iliyoko halmashauri ya wilaya ya Mlele Mkoani Katavi.

Madarasa ya shule ya sekondari kamsisi yaliyojengwa kwa fedha za SEQUIP
ambayo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Sahili Geraruma amesifia ujenzi
wake kuwa wa ubora na viwango vinavyohitajika.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa  Uhuru Kitaifa mwaka 2022, Sahili  Geraruma akizungumza muda mfupi baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa madarasa ya shule hiiyo, ameeleza kufurahishwa na kuridhishwa usimamizi mzuri wa na kaziiliyofanyika ya  ujenzi  na usimamizi wa mradi huo..

Amesema mradi huo wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kamsisi iliyojengwa kwa fedha za Mpango wa Kuboresha Elimu ya Sekondari SEQUIP  ni moja ya  shule bora hapa nchini iliyojengwa na kusimamiwa kwa ubora unaotakiwa.

Katika ujenzi huo umezingatia  viwango vinvyohitajika kwa kuwa tangu ameanza kukagua miradi ya SEQUIP hajawahi kukutana na mradi mzuri na wenyeubora kama huu hongereni sana Mlele alisema kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa.

Amesema katika halmashauri ambayo miradi imependeza ni pamoja na miradihuu, (Secondary Education Quality Improvement Program SEQUIP) ambapo fedhakiasi cha shilingi 565.113 hadi sasa kiasi cha shilingi milioni 512,113,000 kimetumetumika.

Katika hatua nyingine amewataka wataalam kutumia elimu zao walizosomea kwa ajili ya kuiletea maendeleo taifa na waweze kuweka  alama hata kama
wataondoka katika eneo la kazi,taaluma ziongee Katika utendaji kazi wao.

Awali  akisoma  taarifa ya  ujenzi wa shule hiyo Mkuu wa Shule ya Inyonga
Sekondari,Mwl Patrick Kapita ambaye ni ndiye Msimamizi wa  ujenzi wa Shule hiyo alieleza kuwa ujenzi ulianza March,2022 baada ya kupokea fedha kiasi cha shilingi milioni 565,113,000/= kutoka SEQUIP ikiwa ni utekelezaji wa sera ya Serikali inayotaka kila Kata  kuwana shule ya Sekondari.


Mradi huo ulihusisha ujenzi wa jingo la utawala,vyumba vitatu vya maabara za masomo ya sayansi,vyumba vinane vya madarasa ,maktaba moja ,chumba kimoja cha TEHAMA na matundu 20 ya vyoo hadi kukamilika ujenzi utagharimu kiasi cha shilingi milioni 565,113,000 hadi hatua hii iliyofikia kiasi cha shilingi milioni 512,113,000 iko katika hatua za ukamilishaji.

Kukamilika kwa Mradi huo kumeelezwa kutapunguza msongamano wa wanafunzi katika shule mama ya sekondari ya Inyonga unaotokana na ongezeko la ufauluwa wanafunzi.

Leonard Kiyungi akizungumza kwa niamba ya wananchi Kata ya Kamsisi amemushukuru rais Samia Suluhu Hassan kuwaletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na miradi mingine ya maendeleo.

Alieza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo kutasaidia kupunguza mdondoko wa wanafunzi uliokuwepo na hatimaye kuongeza ufaulu.

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages