Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumza namna ambavyo hajaridhishwa na utekelezwaji wa mradi ya umeme wa Gridi ya Taifa. |
Na Walter Mguluchuma,Katavi.
KAMATI ya ushauri ya Mkoa wa Katavi imetoa tamko la kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa umeme wa gridi ya Taifa unao tokea Mkoani Tabora kuwa haidhishi hata kidogo wakati wananchi wanahitaji umeme.
Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Katavi imetoa tamko la kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa umeme wa gridi ya Taifa unao tokea Mkoani Tabora kuwa haidhishi hata kidogo wakati wananchi wanahitaji umeme
Tamko hilo limetolewa wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanavua Mrindoko .
Azimio la tamko hilo limetolewa na wajumbe wa kikao hicho kufuatia taarifa iliyotolewa mbele ya wajumbe wa kikao hicho na Afisa mahusiano wa Tanesco Mkoa wa Katavi Proches Joseph kuwa mradi huo unatarajia kukamilika ifikapo mwezi wa Agosti mwakani na kwa sasa umefikia asilimia 20 .3 upo kwenye usafishaji wa njia za kuweka nguzo na kusambaza .
Kufuatia kutolewa kwa taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameeleza kutoridhishwa na utekelezaji ujenzi wa mradi wa umeme wa Gridi ya Taifa Mkoani Katavi kutokana na kususua utekelezaji wa mradi huo .
Amesema kuwa kasi ya ujenzi wa mradi huo imekuwa ndogo isiyoridhisha kwa kwa kuwa mpaka sasa mradi huo umetekelezwa kwa ailimia 20.3
Amesema kuwa wakati wa ziara ya Makamu wa Rais aliyoifanya Mkoani Katavi aliagiza kuwa mradi huu ukamilike kwa wakati uliopangwa ili wananchi wa Mkoa wa Katavi waweze kupata umeme wa uhakika
Mbunge wa jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso akisema kuwa tatizo la mradi wa umeme sio la gridi ya Taifa hata kwenye mpango wa Rea awamu ya tatu kasi ni ndogo kwani unatakiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani lakini hadi sasa ni vijiji 9 tuu walivyoweka umeme katika
Mkoa mzima kati ya vijiji 52 vya Mkoa huu vinavyotakiwa kupatiwa umeme kwenye aamu hiyo .
Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi alieleza kuwa kasi ya ujenzi wa umeme wa gridi ya Taifa sio ya kuridhisha kwani kinachoinekana kwenye mradi huo ni njia tuu za sehemu watakazo pitisha umeme na nguzo zilizo rundikwa .
Ameshauri kuwa badala ya kuweka nguzo za umeme kwenye mradi huo za miti wangeweka nguzo za zege kwani inashangaza maeneo ya mijini huko wanawake nguzo za zege na kwenye mradi huu unaopita maeneo ya pori wanaweke nguzo za miti ambazo muda wowote zinawza kuungua kwa moto au kuangushwa na wanyama kama tembo .
Wajumbe wa kikao hicho baada ya kuwa wamepokea michango ya wajumbe mbalimbali walitowa taamko la kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo na kuzishauri mamlaka husika kufatilia ujenzi wa mradi huo.