RC MRINDOKO AWATOA HOFU WANANCHI CHANJO YA POLIO ASISITIZA NI SALAMA

 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizindua chanjo ya Polio katika kituo cha Afya Inyonga B Halmashauri ya wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.
(Picha na Walter Mguluchuma)

Na Walter Mguluchuma,Mlele.

MKUU wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa chanjo ya Polio ni salama na haina madhana ya aina yoyote kwa wanao patiwa chanjo hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa chanjo ya Polio ni salama na haina madhana ya aina yoyote kwa wanao patiwa chanjo hiyo.

Mrindoko ametowa kauli hiyo Desemba moja wakati alipokuwa akizindua chanjo hiyo kimkoa uzinduzi huo ambao umefanyika katika kituo cha afya cha Inyonga B.

Amesisitiza kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiwapotosha watu juu ya chanjo mbambali zinazokuwa zinatolewa hapa nchini ikiwepo na chanjo ya Polio.

Amewahakishia wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa chanjo hiyo ya polio na chanjo nyingine ambazo zimekuwa zikitolewa hazina madhara ya aina yoyote ile hivyo wananchi waendelee kuthamini chanjo.

 Amesema Mkoa wa Katavi utahakikisha chanjo hiyo inafanikiwa kwa zaidi ya asilimia mia moja.

Hivyo amewataka kila mzazi anahakikisha mtoto wake anapata chanjo kabla ya kupata maradhi.

Mrindoko alieleza kuwa chanjo hiyo ya polio ni ya nne kutolewa hapa nchini na wala haina madhara yoyote yale

Kwa hiyo wananchi wa Mkoa wa Katavi waachane kabisa na mila potofu chanjo hiyo ni salama.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Suzana Komba alisema jumla ya watoto 285, 800 watapatiwa chanjo hiyo.

Amesema wamepanga kutowa huduma hiyo kwenye maeneo yanayo towa huduma na pia watapita nyumba kwa nyumba ,

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages