Na Walter Mguluchuma,Katavi.
MBUNGE wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi ameomba wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wawekewe na Serikali utaratibu wa kupatiwa mafunzo ya uchimbaji bora wa madini hayo ili waweze kupata uwelewa zaidi utakao wafanya wawe na uchimbaji bora kuliko ilivyo sasa.
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi ameomba wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wawekewe na Serikali utaratibu wa kupatiwa mafunzo ya uchimbaji bora wa madini hayo ili waweze kupata uwelewa zaidi utakao wafanya wawe na uchimbaji bora kuliko ilivyo sasa.
Ombi hilo ametowa wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Katavi (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Mpanda kilichojadili mambo mbali mbali ya maendeleo yanayohusu Mkoa huu na Taifa kwa jumla .
Amebainisha kuwa kumekuwepo na utaratibu kwenye sekta nyingine kama kilimo kuwa wanapatiwa wakulima elimu ya uzalishaji bora wa mazao yao lakini jambo hilo limekuwa halifanyiki kwa wachimbaji wadogo wa madi ya dhahabu ambao ni sehemu kubwa ya waongezaji wa pato la Taifa na ajirakwa watu .
Hivyo ameomba Serikali iwaangalie wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wa Mkoa wa Katavi na wamikoa mingine kunakofanyika shughuli za uchimbaji wa madini unaofanywa na wachimbaji wadogo waweze kupatiwa elimu ya uchimbaji ulio bora .
Kapufi amefafanua kuwa mchimbaji mmoja akipatiwa uwezo wa uchimbaji ulio bora atakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuongeza ajira kwenye nyanja nyingine ndani ya Mkoa huu wa Katavi na nje ya Mkoa .
Ameeleza kuwa kutokana na elimu ya uchimbaji bora ambayo atakuwa amepatiwa mchimbaji inamfanya aongeza kiwango cha madini anayochimba na kumfanya pia aweze kuongeza ajira kwenye sekta nyingine kwani anaweza kuajiri watu hata kwenye kilimo na kwenye sekta nyingine kutokana na miradi mingine ambayo atakayo kuwa ameianzisha kutokana na mauzo ya madini aliyoyauza.
Kuhusu maswala ya afya amesema kuwa ukamilishwaj ujenzi i wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi inayotalajiwa kuanza kazi mwezi Desemba mwaka huu itakuwa ndio mwarobaini kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi .
Hivyo amesisitiza kuwa kwa watumishi wa afya watakao kuwa wanatowa huduma kwenye Hospitali hiyo wanatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa kwani ukimpa mgonjwa lugha nzuri inakuwa ni sawa na kumpatia tiba mgonjwa .
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Katavi Tasca Mbogo amesema kuwa umefika wakati wa kuangalia namna ya kupunguza na kutatua tatizo la upungufu wa walimu katika Mkoa wa Katavi kwani hadi sasa kunajumla ya upungufu wa walimu wa shule za msingi na Sekondari 3,243 katika Mkoa huu.
Ameshauri pia maafisa ardhi wanapo panga miji wasiangalia hali ya vizazi vya sasa mbali wawe wanaangalia na hali ya vizazi vinavyo kuja kwani kumekuwepo na tabia ya maafisa hao kupanga miji kwa kuangalia tuu hali ya sasa tuu bila kuangalia hali ijayo .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kwa upande wake amesema kuwa Mkoa wa Katavi ni ghala la chakula hivyo wananchi wa Mkoa huu waendelee kutumia vizuri mvua zinazo endelea kunyesha .
Amewataka wanachi waendelee kufanya kazi na kuboresha uchumi wao kwani kilimo ni biashara ,hivyoaliwaagiza Wakuu wa Wilaya katika Mkoa huu wahakikishe mbolea ya ruzuku inafika kwa wakati kwa wakulima na bila kuhujumiwa na mtu yetote.