Na Walter Mguluchuma,Katavi.
ZAIDI ya shilingi Bilioni 17 zimetengwa kwa ajiri ya matengenezo ya barabara zinazosimamiwa na TANROADS Mkoa wa Katavi katika kipindi cha bajeti ya mwaka wa fedha wa 2022/2023 huko Zaidi ya shilingi Bilioni 12 zikitoka katika mfuko wa barabara na Zaidi ya Bilioni 4 kutoka mfuko wa maendeleo wa barabara.
Zaidi ya shilingi Bilioni 17 zimetengwa kwa ajiri ya matengenezo ya barabara zinazosimamiwa na TANROADS Mkoa wa Katavi katika kipindi cha bajeti yam waka wa fedha wa 2022/2023 huko Zaidi ya shilingi Bilioni 12 zikitoka katika mfuko wa barabara na Zaidi ya Bilioni 4 kutoka mfuko wa maendeleo wa barabara
Hayo yameelezwa na Meneja wa TANROADS wa Mkoa wa Katavi Mwandisi Martin Mwakabende wakati alipokuwa akitowa taarifa ya utendaji kazi wa TANROADS Mkoa wa Katavi kwenye kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Mpanda kilichoongozwa na Mkuu wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ambae alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho.
Mwakabende ameeleza kuwa jumla ya shilingi Bilioni 17.254 zimetengwa kwa ajiri ya matengenezo ya barabara huku katika ya fedha hizo kiasi cha shilingi Bilioni 12. 743 ni za kutoka katika mfuko wa barabara na kiasi cha shilingi Bilioni 4. 511 ni za kutoka katika mfuko wa maendeleo .
Katika mwaka huu wa fedha Mkoa Mkoa umepanga kutekeleza miradi 39 yenye thamani ya jumla ya shilingi Bilioni 12, 743,441 kwa ajiri ya kufanya matengenezo ya Barabara kuu za Mkoa zenye jumla ya kilometa 1,201 .81pamoja na kufanya matengenezo ya kinga katika madaraja 201.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha bodi ya barabara Mkoa wa Katavi wakifuatilia kikao hicho kwa makini wakati kikifanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi. (Picha na Walter Mguluchuma) |
Kwa upande wa fedha za maendeleo wamepangiwa jumla ya shilingi Bilioni 4.511ambapo kati ya fedha hizo milioni 947 ni kutoka Bodi ya barabara ni kwa ajiri ya ukarabati wa Mkoa na Wilaya zenye urefu wakilometa 19.5 na Bilioni 3.564 ni za kutoka mfuko wa maendeleo ambazo zitakuwa kwa ajiri ya ukarabati wa barabara zaMkoa na Wilaya zenye urefu wa kilometa 65.4
Mwandisi Mwakabende amebainisha kuwa hadi kufikia Novemba 2022 mikataba 39 imekwisha sainiwa tayari na mikataba hiyo imeisha pata msamaha wa kodi na kazi za matengenezo ya barabara zimeanza kutekelezwa .
Amezitaja baadhi ya changamoto zilizopo katika utekelezaji wa kazi zao kuwa ni wananchi kupitisha mifugo barabarani hivyo huchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa barabara ,wananchi kufanya shughuli za kilimo ndani ya maeneo ya hifadhi ya barabara kama vile barabara ya Kagwira kwenda Karema mwambao mwa ZiwaTanganyika .
Changamoto nyingine ameitaja kuwa ni uhaba wa upatikanaji wa kifusi kwa barabara zinazopita ndani ya maeneo ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi sharia ya hifadhi hairuhusu kuchukua kifusi katika hifadhi aliomba kama kuna uwezekana wa TANROADS kuondokana na changamoto hiyo barabara hizo zihudumiwe na Hifadhi zaTaifa .
Amesema baada ya kufanyika kwa matengenezo ya barabara za Mkoa huu na zinazounganisha na mikoa mingine na Wilaya na Wilaya na kuwa na barabara zenye unafuu huduma ya mabasi imeongezeka pamoja na nauli kupungua .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanavua Mrindoko amewaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa Mkoa wa Katavi umefanikiwa sana kwenye maswala ya sekta ya barabara kwa upande wa usafiri na uchukuzi kwani Serikali imeendelea kutenga bajeti na kutekeleza kwa kiwango kikubwa.
Hali hiyo imeufanya mkoa wa Katavi kuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya barabara na kuufanya kufika kwa urahisi Zaidi kupitia barabara zote zinazounganisha mkoa huo na mikoa mingine pamoja nan chi za Kongo na Burundi.
Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi ameomba fedha zinazotolewa na Serikali zinazotokana na tozo kwa ajiri ya barabara zinazosimamiwa na TARURA zigawanywe kwa usawa kwa kila Halmashauri wasiangalie kama kuna miradi mingine ya wafadhili inayotekelezwa kwenye Halmashauri nyingine .
Amesema katika fedha za tozo zilizopelekwa kwenye halmashauri za Mkoa huu ni Halmashauri yake pekee ya Manispaa ya Mpanda iliyopewa kiasi cha shilingi bilioni moja wakati Halmashauri nyingine za mkoa huu walipatiwa kiasi cha shingi bilioni moja na nusu sababu ya Halmashauri yake kuwa fedha ndogo ilidaiwa ni kwa kuwa wanayo miradi mingine jambo ambalo sio sawa kwani kadi wananchi wote wanatozwa sawa sawa bila kujali wa halmashauri ipi.