MIRADI 19 YA THAMANI ZAIDI YA BILION 4 YAFUATILIWA NA TAKUKURU KATAVI


Makao Makuu ya ofisi ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa - TAKUKURU Mkoa wa Katavi

Na Walter Mguluchuma,Katavi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa imefatilia utekelezaji wa miradi 19 yenye thamani ya zaidi ya BILIONI 4 katika sekta za ujenzi , elimu na afya katika kipindi cha miezi mitatu ya kuanzia Julai hadi Septemba 2022.11.8

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi,Faustine Maijo akizungumza na Wanahabari ofini kwake leo mapema  wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa imefatilia utekelezaji wa miradi 19 yenye thamani ya zaidi ya BILIONI 4 katika sekta za ujenzi , elimu na afya katika kipindi cha miezi mitatu ya kuanzia Julai hadi Septemba 2022.11.8

Hayo yameelezwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi Fautine Maijo wakati alipokuwa akitowa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya kuanzia julai 2022 hadi Mwezi Septemba .

Amebainisha kwa kuzingatia kwamba miradi mingi ya maendeleo ni mali ya wananchi na Serikali inapelela fedha nyingi katika eneo hilo Takukuru Mkoa wa Katavi imefatilia utekelezaji wa miradi 19 yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.5 iliyofuatiliwa katika kipindi hicho .

Maijo ameitaja miradi hiyo waliofatilia kuwa ni ujenzi wa majengo matano ambayo ni Bohari ya dawa , jengo kufulia nguo , jengo la utawala na jengo la mama na mtoto katika Halmashauri ya Nsimbo miradi hiyo mitano imegharimu kiasi cha shilingi Bilioni moja .

Miradi mingine ni ujenzi wa jengo la wagonjwa la dharula Hospitali ya Nsimbo , ujenzi wa kituo cha Afya Itenka ,ujenzi wa kituo cha Afya Town Clinic,ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kapalala , ujenzi wa shule ya sekondari Tanganyika , ujenzi wa jengo la ICU na nyumba za watumishi Hospitali ya Tanganyika na mradi wa maji katika Kijiji cha Vikonge na kufanya thamini ya miradi hiyo kuwa ya Bilioni 4.5,

Baadhi  ya Wanahabari wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa takukuru Mkoa wa Katavi,Faustine Maijo

Amesema kuwa katika miradi hiyo kuna mapungufu madpgo madogo yaliyobainishwa ikiwa ni pamoja na kuchelewa kukamilika kwa miradi kwa mujibu wa mikataba jambo ambalo limesababisha kuongezeka kwa gharama zaidi ya bei ya soko .

Amefafanua kuwa miradi miwili iliyoonekana kuchelewa na ucheleweshaji hivyo uchunguzi umeanzishwa ili kubaini sababu za ucheleweshaji ili kuchukua hatua stahiki dhidi ya watu watakaoonekana kusababisha ucheleweshaji huo ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria .

Pia katika kufatilia fedha za UVIKO 19 baadhi ya shule shikizi zilikamilika na miundo mbinu iliyojengwa kutokana na fedha hizo kuanza kutumika kuwahudumia wanafunzi baadhi ya miundo mbinu imelalamikiwa na kuonekana kuna haja ya kufanyiwa uchunguzi .

Amesema chunguzi hizo bado zinaendelea ili kujiridhisha ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kwa wale wote watakao bainika kufanya makosa yoyote ya jinai kwenye miradi hiyo iliyotokana na fedha za UVIKO 19.

Aidha Takukuru Mkoa wa Katavi imefanya ufatiliaji wa miradi yote iliyozinduliwa na mbio za Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2022 zilizoongozwa na Sahili Geraruma.

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages