WANANCHI NSIMBO WAMEKIRI TASAF KUWAKWAMUA KWENYE UMASIKINI

Nyumba (pichani ya kushoto) ni Makazi ya zamani ya mnufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini-TASAF,Bi Sikuthani Thabiti mkazi wa kijiji cha Tumanini Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi ambapo baada ya kuingia kwenye mpango wa TASAF amejenga nyumba nzuri (pichani ya kulia).

MAKALA KWA UFUPI.

Sikuthani Thabiti,Mkazi wa kijiji cha Tumaini Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi amekiri kupata maendeleo makubwa kupitia TASAF,ambapo ameweza kusomesha watoto wake wawiili ,wenye umri wa miaka 17 na wa mwisho miaka 14 ikiwa mbali na kusomesha watoto anasema kupitia fedha za TASAF ameweza kujenga nyumba na kuimarisha makazi yake ya kuishi.

Na George Mwigulu.

Sikuthani Thabiti,Mkazi wa kijiji cha Tumaini Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi amekiri kupata maendeleo makubwa kupitia TASAF,ambapo ameweza kusomesha watoto wake wawili wenye umri wa miaka 17 na wa mwisho miaka 14 ikiwa mbali na kusomesha watoto anasema kupitia fedha za TASAF ameweza kujenga nyumba na kuimarisha makazi yake ya kuishi.

Anasema “Hapo awali kabla ya kupewa fedha hizo za TASAF ndugu zangu nilikuwa na maisha magumu,niliishi kwenye nyumba ya miti kama mnavyoona na nilishindwa kumudu gharama za kuwanunulia sare za shule watoto wangu”.

Naye Suzana Rashidi (40),Mkazi wa kijiji cha Itenka “A” Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi anasema TASAF kupitia serikali imemsaidia kumtoa kwenye janga la ufukara ambapo yeye na familia yake aliishi bila kuwa na matumaini kwamba siku moja watakuja kuondokana nayo.

Ameweka wazi kuwa kabla ya hajaingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini-TASAF suala la kujikimu milo mitatu ilikuwa ni ngumu licha ya kufanya kazi ngumu za vibarua kwa watu hakuweza kumudu gharama za maisha ya kila siku.

Aidha anaeleza,mara baada ya kuingizwa kwenye mpango ambao hakutarajia kutokea maishani mwake  mwaka juzi alianza kufanya biashara ndogo ndogo ya kupika maandazi na kuuza chai,ambapo alipolipwa fedha za awamu ya kwaza kwake alienda mashineni za kukoboa mpuga na kununua chenga za mchele kama kg 30  na mafuta lita 3 na kuandaa maadazi hayo na kuuza kwa kutembeza kwenye majumba ya watu kijijini hapo.

Mwanamke huyo ambaye ameonekana mwenye uso wa furaha anakiri wazi pasipokuwa na shaka kuwa mpango wa kunusuru kaya masikini –TASAF ni mwarobani wa maisha yake magumu aliyowahi kuyapitia hapo awali na kwamba kwa sasa ameweza kumudu gharama za maisha na kuweza kusemesha watoto wake wane shule.

Sambamba na hayo ametoa rai kwa jamii na serikali  kuendelea na TASAF kwa nia njema ya kuwakwamua watu wenye maisha magumu kuondokana na taabu ambazo zinazorotesha ukuaji wa uchumi kwao na kwa taifa kwa ujumla.

Amesisitiza “natoa shukrani zangu za dhati kwa serikali ndugu mwandishi naomba uzifikishe kwa rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassain, nazidi kuomba wasituache bali waendelee na moyo huo huo wa kutusaidia  ili tuweze kulea watoto wetu ambapo tuliachwa kwa hila na waume zetu”.

Mtu mwingine Joyce Aloyce Mkazi wa Kijiji Cha Katambike Kata ya Ugalla  alipoliona gari ambalo hutumika kwenye uhaurishaji fedha kwao alilisimamisha na kuanza kuongea na Mratibu wa TASAF halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,Frankson Kalugendo alimwambia kuwa anaamini bila kuwa kwenye mpango huo maisha yake yangekuwa magumu sana na pengine angepata athari  za kiafya kutokana na kufanya kazi ngumu.

Nyumba ya mmoja wa wanufaika wa TASAF Bi Sikuthani Thabiti Mkazi wa Kijiji cha Tumaini halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi.

Katibu Usitawi wa Kijiji cha Mnyamasi halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi Andrew Issa anasema kuwa jamii imeshaondokana na imani potofu juu ya uhawirishaji wa fedha za TASAF ambapo jamii ilikuwa ikidhani pesa hizo sio salama.

Ameeleza kuwa kuwa mwitikio umekuwa mkubwa sana kwa jamii kiasi kwamba kuna mabadiliko makubwa sana ya ukuaji kiuchumi kwa watu maana wanapopokea fedha hizo wengi wao wamekuwa wakizielekeza kwenye uzalishaji wa kilimo,ufugaji na biashara.

Mratibu wa Mpango wa kunusuru Kaya masikini – TASAF halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Frankson Kalugendo  amesema jumla ya vijiji 54 vya halmashauri hiyo vinawalengwa wa TASAF ikiwa na walengwa 3000 wakipokea fedha kwa njia tofauti tofauti kama vile Cash,Mtandao (Bank) wanapokwenda kulipa wanakuwa na mawakala na wanalipa kwa njia ya simu.

Kaludendo amefafanua kuwa kwa wanufaika wa TASAF wanaendeleo kuona mafanikio makubwa wakiyapata kwa jinsi wanavyozipokea na kuzitumia licha ya kwamba halmashauri hiyo inatekeleza Component chache ikiwemo uhaurishaji fedha ambayo ni ruzuku ya msingi pamoja  na fedha ya masharti.

Aidha amezidi kutoa wito kwa wanufaika wote wa TASAF kuzigaitia matumizi bora ya fedha hizo licha ya kuwa wamepiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages