WALIOPINGA IMANI POTOFU JUU YA TASAF WATOKOMEZA UMASIKINI MPANDA

 

Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Joshua Willian Sankala akizungumza hivi karibuni na baadhi ya wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya masikini waliopo Kata ya Kakese.


MAKALA KWA UFUPI

Imani potofu kuhusu uhawilishaji fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF kwa kaya masikini umeondoka katika vijiji vya Mkwajuni na Kabwaga Kata ya Mwamkuru Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi baada ya kujionea jinsi ambavyo walengwa wa mpango huo wa kunusuru kaya masikini wanavyojinasanua kwenye wimbi la umasikini.

Huu ni mwonekano  wa nyumba ya mnufaika wa mpango wa kunusu kaya masikini - TASAF,Suzana Mapesa kutoka kijiji cha Kabwaga Kata ya Mwamkuru Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Na George Mwigulu

Imani potofu kuhusu uhawilishaji fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF kwa kaya masikini umeondoka katika vijiji vya Mkwajuni na Kabwaga Kata ya Mwamkuru Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi baada ya kujionea jinsi ambavyo walengwa wa mpango huo wa kunusuru kaya masikini wanavyojinasanua kwenye wimbi la umasikini.

Hayo amesema hivi karibuni mnufaika wa mpango wa TASAF na Mkazi wa Kijiji cha Mkwajuni,Cosmas Lazaro (34) wakati akizungumzia hali yake ya maisha ya kabla na baada ya kuingizwa kwenye mpango wa TASAF ambapo amesema wakati mpango huo unaingia kijijini kwao kulikuwa na woga mkubwa wa kaya masikini kukubali kuingizwa.

“hivi kweli serikali inaweza kutoa hela za bure.hapana hii ni freemason kabisa na watakao ingia kwenye mapango huo watauganishwa bila wao kufahamu “ amesema Cosmas.

Mnufaika huyo wa TASAF anaeleza kuwa kaya masikini nyingi zilikataa kujiunga na mgango huo na hata kama walikubali kuandikishwa majina yao kwenye mpango wengi wao walidanganya majina kwa kuandika majina ya watu ambayo wala hayafahamiki.

Anasema “nikuambie mwandishi kipindi hicho mtu anadanganya kwa kuandikisha jina kwa mfano Anthony Nyango kumbe jina lake ni Gigwa Masala…Hiii! Ngoma ilikuwa nzito pale sasa wawezeshaji walipokuja kutoa fedha hizo maana litaitwa jina la Anthony Nyango na aliyeliandikisha jina hilo naye kashasahau hilo jina kwa sababu alitamka kwa uwongo”.

Cosmas Lazaro mkazi wa kijiji cha Mkwajuni Kata ya Mwamkuru Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi akielezea namna ambavyo Imani potofu imefutika kijiji kwao na wananufaika na mpango wa TASAF.

Hali hiyo ilibadilika ghafura baada ya wanufaika wa TASAF kuanza kubadili maisha yao, Akizungumzia maisha yake Cosmas anasema kuwa yeye ni mtoto yatima aliishi na dada yake kwa muda mrefu wakiwa na maisha duni na wakati mwingine hawakuweza kupata chakula hata mlo mmoja kwa siku.

Amesema kuwa baada ya kuingizwa ndani ya mpango mambo yamebadirika sana kiasi kwamba fedha anayoipata ameweza kuwekeza saloon ya kunyolea nywele sambamba na ufugaji wa kuku ambao umemwezesha kujenga nyumba za kuishi nzuri tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Maneno yake yamenda sambamba na Suzana Mapesa ambaye ni mnufaika wa mpango wa TASAF na mkazi wa kijiji cha Kabwaga ambapo anasema kuhusu Imani potofu kuhusu TASAF ilikuwa kikwazo kwa kaya masikini ambazo ziliogopa kuuganishwa kwenye mpango.

Suzana anaeleza kuwa mambo yamekuwa tofauti kwa sasa kwa sababu yeye na kaya zingine ambazo zimeugwa kwenye mpango huo zimepiga hatua kubwa sana za maendeleo ikilinganishwa na hapo awali,Hivyo wamekuwa chachu ya kaya zingine masikini kuondokana na Imani hizo na kuamua kujinga na TASAF.

Nyumba (kwenye picha ya kwanza kulia) ya Suzana Mapesa mnufaika wa TASAF na mkazi wa kijiji cha Kabwaga ndio nyumba yake amejenga baada ya kuingia kwenye mpango wa TASAF ambapo nyumba (kwenye picha ya kwanza kushoto)ni nyumba yake ya kabla  kuingizwa kwenye mpango.

“nikuambie walipokuwa wakiona nyumba hii nzuri macho yaliwatoka wote waliojifanya wana Imani zao potofu kuhusu fedha za TASAF,hawakutegemea wakilinganisha na maisha yangu ya hapo kabla ya mpango jinsi ambavyo yalikuwa magumu” anasema Suzana.

Suzana anasema kuwa jamii inapaswa kuacha kutilia shaka nia njema ya serikali ya kuwasaidia watu wake kwa sababu malengo ya TASAF ni kuondoa umasikini wa kaya masikini.

Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kabwaga,Godfrey Madima amesema kuwa ni kweli kwenye mwaka wa  2020,April ili kulikuwa na changamoto kubwa ya watu kuwa na Imani potofu na kuandisha majina ambayo sio ya kwao ambapo baada ya taratibu kubadilika kwa kutumia vitamburisho vya utaifa kaya 70 ziliweza kuondolewa na kubakia kaya 24 pekee kwa sababu majina yao hayakuendana na vitamburisho vyao.

Kwa sasa anasema kaya masikini zimetambua kuwa ndani ya TASAF kuna fursa kubwa ya kuinua maisha yao baada ya kujifunza kutoka kwa wanufaika wengine ambao wameweza kumudu shughuri za kilimo na wengine kujenga nyumba bora za makazi ambapo kila wakati wanauliza ni lini tena wataweza kusajiliwa kwenye mpango wa TASAF.

 




Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages