MKAZI WA KATAVI KIZIMBANI KWA KOSA LA KUFANYA TENDO LA NDOA NA MTOTO WAKE.


Na Walter Mguluchuma,Katavi.

Boda boda  Idrisa  Said  Bayaga(32) wa Kituo cha  waendesha pikipi cha Nyerere Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi amefikishwa kizimbani kwa tuhuma za kufanya(mapenzi) tendo la ndoa(MAHARIMU)na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe mwenye umri wa (11).

Boda boda  Idrisa  Said  Bayaga(32) wa Kituo cha  waendesha pikipi cha Nyerere Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi amefikishwa kizimbani kwa tuhuma za kufanya( mapenzi)  tendo la ndoa(MAHARIMU )na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe mwenye umri wa (11)

Mtuhumiwa huyo amekishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Hakimu  mfawidhi mwandamizi  Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Gosper Luoga .

Mwendesha mashitaka mwanasheria wa Serikali  Gregoli  Mhangwa  ameiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la kufanya mapenzi na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe kwa nyakati tofauti kuanzia kipindi cha mwezi  April   mwaka huu hadi  mwezi septemba .

Aidha kuwa kitendo hicho  cha  kufanya tendo la ndoa na mtoto wake mwenye umri mdogo wa miaka 11  ni kutenda kosa kinyume na kifungu cha sheria Namba 158(1) (a) cha kanuni  ya  adhabu  sura  16 kama ilivyofanyiwa marekebisho 2019.

Mtuhumiwa huyo baada ya kusomewa mashitaka hayo  na mwanasheria wa Serikali alikana na mashitaka hayo ya kutenda kosa la kufanya tendo la ndoa    kwa  nyakati tofauti na mtoto wake wa kumzaa  mwenyewe.

Baada ya mtuhumiwa kukana mashitaka hayo mwendesha mashitaka  Gregoli  Mhangwa  aliiambia  Mahakama kuwa upande wa mashitaka umeisha kamilisha  upelelezi wa kesi hiyo .

Hivyo aliiomba Mahakama iweze   kuendelea na hatua zinazofuata  za kimahakama kufuatia kukamilika kwa  upelelezi uliofanywa na pande wa mashitaka .

Kufutia maombi hayo ya upende wa mashitaka Hakimu Luoga alikubaliana na hoja hiyo iliyotolewa mbele yake na upande wa mashitaka  ambapo mtuhumiwa  Idrisa  Said  Bayaga alisomewa  hoja za awali za mashitaka .

Baada ya kutolewa mahakamani hapo hoja za awali  kuwasilishwa Mahakani hapo  Hakimu Mkazi mfawidhi  Mwandamizi Gosper Luoga  aliiambia mhakama kuwa mdhamana wa mshitakiwa upo wazi na anatakiwa awe  na mdhamini mmoja mwenye mali isiyo hamishika na dhamana kuwa wazi Huku mtuhumiwa  kushindwa kutimiza mashariti hayo .

Kesi hiyo imeharishwa hadi hapo Desemba 5 itakapoanza kusikilizwa  ambapo  mtuhumiwa amekwenda rumande kwenye gereza la mahabusu la Mpanda Mjini.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages