WANA-UVINZA WASHITUKA UPIMAJI WA VIJIJI KUTAIFISHA MAENEO YAO KUWA USHOROBA

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Lubufu Kata ya Kalya Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye kikao cha kujadili tatizo linaliwakabiri la baadhi ya maeneo yao kuwekewa bikoni kuwa sehemu ya Ushoroba.

 Na Paul Mathias,Uvinza.

Wananchi wa Kijiji cha Lubufu Kata ya Kalya Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma wameiomba serikali iwaluhusu kuendelea kuyatumia maeneo yao ambayo wamekuwa wakifanya Shughuli za kilimo na makazi kwa muda Mrefu ambapo hivi karibuni maeneo hayo yamewekewa Bikoni kama Ushoroba wa wanyama bila kushirikisha Uongozi wa Serikali ya Kijiji hicho.


Wananchi wa Kijiji cha Lubufu Kata ya Kalya Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma wameiomba serikali iwaluhusu kuendelea kuyatumia maeneo yao ambayo wamekuwa wakifanya Shughuli za kilimo na makazi kwa muda Mrefu ambapo hivi karibuni maeneo hayo yamewekewa Bikoni kama Ushoroba wa wanyama bila kushirikisha Uongozi wa Serikali ya Kijiji hicho.

Amos Faustine,Mkazi wa kijiji hicho amesema kuwa wameshangazwa na kuona maeneo yao yakiwekewa Bikoni bila kushirikishwa hali ambayo imewaweka katika mashaka makubwa kutokana na kukaa katika maeneo hayo kwa muda mrefu.

Ameeleza kuwa baada ya kuona hali hiyo wananchi walimua kuitisha kikao cha dharula kwa ajili ya kujadili swala hilo ambalo hawakulitalajia hali ambayo iliwalazimu Kuteua Kamati ya watu watatu kufika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Uvinza ili kujua ukweli wa jambo hilo.

Faustine amesema kuwa walipofika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza na kuonana na Mkuu wa wilaya hiyo Hanafi Hassain Msabaha  amekana taarifa hiyo na kusema yeye hajatuma Maafisa wake kwa ajili ya kuweka mapitio ya wanyama isipokuwa alituma watu kwa ajili ya kuweka mipaka  kati ya ya kijiji na Kijiji.

Mkazi huyo wa kijiji cha Lubufu amefafanua kuwa Shoroba zinazojulikana  katika kijiji hicho ni pamoja na mapitio yaliyopo katika Vijiji vya Mjimwema, Mapanda ambayo ni njia kuelekea kijiji cha Sulwa, Hadi kaza buti na Kawilimile na kwenda kuungana na Mbuga ya hifadhi ya wanyama ya Katavi ambapo amewaomba viongozi na mamlaka kushughurikia tatizo hilo kwa muda muafaka.

Michael Bulugu,Mkazi wa kijiji cha Lubufu Kitongoji cha Lugaraba amesema maeneo hayo wamekuwa wakiyatumia kufanya kazi mbalimbali tangu mwaka 1974 na kuna wazazi wao ambao wapo katika maeneo hayo tangu mwaka huo na hawajahama kwenda sehemu nyingine kutokana na maeneo hayo kuwa maeneo ya miliki yao halali tangu wakati huo.

Bulugu ameshangazwa kuambiwa kuwa maeneo hayo ni sehemu ya Mapito ya wanyama Shoroba huku maeneo ya shoroba katika kijiji hicho yanajulikana hivyo anawasiwasi na viongozi wa serikali ya kijiji  kwa kuwa na dalili za kutokuwa na mshikamano kwenye  kuwatumukia wananchi waliowachagua.

Amefafanua kuwa viongozi hao ndio waliowauzia maeneo hayo na kuwaruhusu kufanya makazi na shughuli zingine ikiwemo kilimo na ufugaji hivyo wanasikitishwa na hatua hiyo na kuiomba serikali kuingilia kati swala hilo ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao kwenye  msimu huu wa mvua kunyesha.

Mwenyekiti wa Kjiji cha Lubufu Juma Kapingu Magembe amesema kuwa suala hilo limekuja kwa mtizamo wa Vijiji kupimwa ili kuwekewa mipaka ya kijiji ambapo kwenye  zoezi la mara ya kwanza kufanyika viongozi wa kijiji walishirikishwa zoezi hilo ila kwa muda huu imekuwa tofauti kwa zoezi hilo kufanyika bila kushirikisha  viongozi.

Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa wananchi hao kwa mara kadhaa wamekuwa wakipata wasiwasi kuhusiana na swala hilo huku viongozi wa kijiji hicho wakiwa wamepanga kwenda kuonana na uongozi wa ngazi za juu ili kuona ufumbuzi wa tatizo hilo. 

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma,Hanafi Hassain Msabaha licha ya  kutafutwa na blog hii kwa kupigiwa simu na kutumiwa meseji hakuweza kupokea simu wala kujibu meseji ili kuweza kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wananchi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages