TASAF YACHOCHEA UKUAJI SEKTA YA KILIMO HALMASHAURI YA NSIMBO

Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Frankson Kalugendo (wa kwaza kulia) akizungumza na mnufaika wa mpango huo,Bi Marry Kanija mkazi wa kijiji cha Tumaini ambapo alieleza namna ambavyo mchango wa TASAF umeweza kuwainua kimaisha.

Na George Mwigulu.

Katika kuboresha sekta ya kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Mpango wa kunusuru kaya masikini- TASAF umetoa mchango mkubwa hasa kwa kaya masikini ambazo kumudu gharama za kilimo ilikuwa ngumu kutokana na uduni wa maisha.

Nyumbani kwa mnufaika wa mpango wa TASAF,Marry Kanija ambaye ni mkazi wa kijiji cha Tumanini Halamashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi. (Kushoto ni nyumba iliyoezekwa kwa bati za kisasa maarufu Msauzi aliyoijenga kupitia TASAF baada ya kuwekeza kwenye kilimo na mbele yake ni nyumba ambayo baada ya kuingia kwenye mpango alijenga na kuezeka kwa bati za kawaida)

Katika kuboresha sekta ya kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi,Mpango wa kunusuru kaya masikini- TASAF umetoa mchango mkubwa hasa kwa kaya masikini ambazo kumudu gharama za kilimo ilikuwa ngumu kutokana na uduni wa maisha.

Marry Kanija,Mkazi wa Kijiji cha Tumaini kilichopo katika halmashauri hiyo ambaye pia ni moja ya wanufaika wa mapango wa TASAF amesema hayo hivi karibuni nyumbani kwake baada ya kutembelewa na Mratibu wa Tasaf Frankson Kalugendo na timu ya waandishi wa habari ili kufuatilia wanufaika hao.

Amebainisha kuwa kaya masikini ziliachwa nyuma sana kwenye sekta ya kilimo kutokana na hali halisi ya maisha yao kuwa duni ikilinganishwa na gharama zilizopo za uendeshaji wa kilimo kuwa za juu sana na kushindwa kumudu.

Mnufaika wa mpango wa TASAF huyo amesema gharama kubwa za kununulia pembejeo kama vile mbolea,viuwatilifu,gharama za kukodishia mashamba na gharama za kulipa vibarua vilikuwa

vikwazo ambavyo vilipelekea kushindwa kufanya kilimo.

“…mtu yeyote yule kwa mazingira yetu ya vijijini asiyeweza kujishughurisha na kilimo ni lazima maisha yake yatakuwa ya tabu,itakuwa rahisi kukosa chakula cha milo mitatu na hata wakati mwingine atashindwa kujinunulia mavavi na kukosa makazi mazuri ya kuishi” amesema Marry.

Amesisitiza “ utafanya nini kama huna pesa za kuwekeza kwenye kilimo!. Matokeo yake utafanya kibarua kwa ajili ya kuwazalishia watu wengine…tizama kwa sasa baada ya kuingizwa kwenye mpango wa TASAF ninaweza kuweka akiba kidogo kidogo ambacho kinaniwezesha kumudu gharama za kilimo”.

Kiasi ambacho alianza nacho kupokeani Tsh 36,000/= hadi sasa kimefikia Tsh 46,000/= na kwamba yuko ndani ya mpango wa TASAF kwa miaka mitatu na fedha ambazo amezipata yeye na familia yake kwa kuwekeza kidogo kidogo zimemsaidia kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo.

Ameeleza kuwa haikuwa rahisi suala la matumizi bora ya fedha na kwamba inahitaji usubutu kutoka moyoni kuwekeza kwenye kilimo ambacho kimemfanya kuvuna zaidi ya gunia 40  kwa ekari mbili na sasa ni miaka mitatu anajishughurisha kwenye kilimo ambacho kupitia TASAF kimemkomboa na amejenga nyumba nzuri.

Aidha amesema kupitia TASAF kaya nyingi masikini zimejikwamua kwenye kilimo na kuwa mfano bora kwa ndani ya jamii yao ambayo hapo awali iliwaona kama watu wavivu na wasio kuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote la kimaendeleo.

Nyumba ya Marry Kanija (kwenye picha) mkazi wa kijiji cha Tumaini akiwaonesha nyumba yake aliyoijengwa na kuienzeka kwa bati za kisasa maarufu kwa jina la Msauzi.

Happyness Masala ambaye naye ni mnufaika wa pango wa kunusuru kaya masikini TASAF amesema kuwa wanufaika wengi wa mpango huo TASAF imekuwa chachu ya ukuaji wa sekta ya kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo kwa kuwa ni chemchem ya kipato cha fedha ambacho kinawasaidia kuwekeza kwenye kilimo.

Mnufaika huyo amesema “tembelea halmashauri yote hii utajionea mwenyewe namna ambavyo wanufaika wengi wa mpango wa TASAF walivyo piga hatua kwenye sekta ya kilimo…utaona wako mashabani wakati wa mvua na wanavuna gunia nyingi za  mpunga na mahidi kiasi kwamba wamepiga hatua ya kila mmoja kujenga nyumba nzuri kwa ajili ya makazi.

Kwa upande wa Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Paul Cheyo akizungumzia kwa ujumla mchango wa TASAF kwenye sekta ya kilimo  amesema licha  ya msimu wa kilimo uliupita kuwa na changamoto ya mvua lakini kwa msimu wa 2021/22 malengo ya uzalishaji halisi ulimuwa Tani 75,235 na utekelezaji halisi ulikuwa Tani 54,948 sawa na asilimia 73 ya lengo.

Afisa kilimo huyo amesema kuwa uzalishaji haukufanikiwa kutokana na hali mbaya ya hewa ambapo atawanyiko wa mvua ulikuwa mbaya kwani mvua hazikunyesha kwa wakati na tena zilikuwa chache  lakini wanatambua mchango mkubwa TASAF kwenye kuinua sekta ya kilimo halmashaurini hapo. 

Cheyo amefafanua kuwa mchango wa TASAF ni mkubwa sana kwa kaya masikini ambazo zilikuwa hazikopesheki na taasisi za kifedha,TASAF imebeba dhamana hiyo kwa kutoa fedha ambazo zimewasaidia kununua mbolea za kilimo kitu ambacho hapo awali hawakuweza kumudu kutokana na ukata wa fedha ambao waliokuwa nao.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages