KAIMU MKUU WA GEREZA LA MAHABUSU MPANDA ATOA SHUKRANI KWA MBUNGE.


Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini,Sebastian Kapufi (Kwaza kushoto) akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa Kaimu Mkuu wa  Gereza la Mahabusu Mpanda,Christopher Fungo.

Walter Mguluchuma na Paul Mathias.

Kaimu Mkuu wa Gereza Mahabusu la Mpanda amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi kwa kuguswa na kuona kushirika  katika mwaka mpya kwa kushiriki na Jamii iliyotegwa kwa Mjibu wa sheria na jamii waliohukumiwa na wengine wakisubilia vifungo vyao kwa kuwapatia Mahitaji mbalimbali ikiwemo Chakula.

Kaimu Mkuu wa Gereza la Mahabusu Mpanda,Christopher Fungo akitoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini,Sebastian Kapufi baada ya kukabidhiwa mahitaji mbalimbali.
Kaimu Mkuu wa Gereza Mahabusu la Mpanda amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi kwa kuguswa na kuona kushirika  katika mwaka mpya kwa kushiriki na Jamii iliyotegwa kwa Mjibu wa sheria na jamii waliohukumiwa na wengine wakisubilia vifungo vyao kwa kuwapatia Mahitaji mbalimbali ikiwemo Chakula.

Shukurani hizo zimetolewa na Kaimu mkuu wa Gereza la mahabusu Mpanda Christpher Fungo mara baada ya kupokea msaada huo aliokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Mpanda mjini  Sebastiani  Kapufi.

Alisema kuwa bado wanaendelea kuhitaji misaada mingine na tunashukuru kwa kuguswa na kutambua kuwa wenzetu hawa wanahitaji vitu kama hivyo.

Ameeleza kuwa mbunge huyo amejinyima kwa moyo wa dhati kwa kujitolea kwa niaba ya watumishi wa magereza anaomba msaada huo usiishie hapo bali uwe endelevu kwao.

Kwa pande wake Mbunge wa Jimbo la Mpanda mjini Sebastiani Kapufi amesema ameguswa kwa  kuamini kuna wenzetu wa Magereza na watoto yatima kwa namna ambayo mwenyezi mungu amemjalia na wakati tukienda kuupokea mwaka mpya 2023 amewiwa kuwatembelea na kutoa vitu mbalilmbali.

Alisema ametoa zawadi ya Vitu mbalimbali ikiwemo Mafuta ya Kupikia, Sabuni ,Mchele, Taulo za kike,Dawa za meno ,Nyama ya Ng’ombe na Vinywaji baridi.

Moses Mbesella Mkuu wa Gereza la Mahabusu Mpanda anaemaliza utumishi wake wa umma akitoa maneno ya shukrani.
Nae Moses Mbesella Mkuu wa Gereza anaemaliza utumishi wake wa umma amesema anakila sababu ya kumshuru Mbunge kapufi kwa msaada alioweza kuutoa nakuona kwamba mahabusu na wafungwa wanahaki ya kuuona mwaka mpya kwa kupata mahitaji kama hayo.

Ameeleza kuwa mbunge huyo amekuwa mbunge wa muda mrefu na analijali sana Gereza la Mahabusu Mpanda na tunamwombea kwa mwenyezi mungu aendelee kumujalia moyo wa ukalimu alisema Moses. 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages