Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini,Sebastian Kapufi (kushoto) akisalimiana na Sister Rose Sungura.
Na Walter Mguluchuma,Mpanda.
Watoto yatima waliopo katika kituo cha kulea watoto cha Mtakatifu Yohane Paul wa pili Matumaini ya watoto kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi wameshukuru Msaada ulitoewa na Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi kwaajili ya sikukuu ya mwaka mpya.
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini,Sebastian Kapufi akizungumza na waandishi wa habaei mara baada ya kumaliza kutoa mahitaji mbalimbali.
Watoto yatima waliopo katika kituo cha kulea watoto cha Mtakatifu Yohane Paul wa pili Matumaini ya watoto kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi wameshukuru Msaada ulitoewa na Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi kwaajili ya sikukuu ya mwaka mpya.
Akipokea
zawadi hizo kwa niaba ya watoto hao Mkuu wa kituo hicho Sisiter Rose Sungura
amesema wamepokea zawadi ya vitumbambali kutoka kwa Mbunge huyo kwa mikono miwili.
Amesema kuwa
kituo hicho kilianzishwa mwaka 2019 na
Mpaka sasa kimeshapokea jumla ya Watoto 50 ambapo watoto walipo kwa sasa
kituoni hapo ni watoto 21.
Kituo hicho
kimeanza kukua hii inatokana na mapokea mazuri ya Jamii ya watu wa Mpanda kwa
kuendelea kukilea na kukitunza kituo hicho na mungu awabariki sana.
Amesema
mbunge huyo ametenda tendo jema sana na mungu amemuona na aendelee kuwaona watu
wake wa Mpanda kwa kama jinsi alivyowaona watoto hao.
Kwa upande
wake Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi ameguswa kwa kuamini
kuna watoto yatima na magereza kwa kuwapatia chakula na mahitaji ya vitu
vingine.
Amebainisha kuwa alipokuwa Magereza ameobwa afikishe salamu zake za upendo kwa umma kuwa kuwa Gerezani siomwisho wa maisha na eneo hilo mtuyeyote anaweza akafika huko.
Kubwa walilomweleza wanasema wataendelea kuwa watu wema na hata wao wanaweza wakawa wabunge watalajiwa na wameomba watakapomaliza kifungo chao jamii iwapokee kwakuwa watakua wameshakuwa watu wema.Ukiacha
wafugwa kuna watoto yatima ambapo amefika hapo na kuwasaidia mahitaji kidogo
aliyojaliwa na mwenyezi Mungu kwa kuwapatia Pampas,Maziwa ya kopo
lactrogen,Mchele na mafuta ya Mawese pamoja na nyama.
Pamoja na kutoa msaada kwa Magereza na wafungwa na kituo cha watoto cha mtakatifu Yohane anatalajia kutembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa katavi na kuwafariji wagojwa kwa kuwapatia vitu mbalimbali.