![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nsemlwa Manispaa ya Mpanda Mkoani hapo wakati akikabidhiwa vyumba vya madarasa (Picha na George Mwigulu) |
Paul Mathias,Mpanda.
Serikali ya Mkoa wa Katavi imesema haita mvumilia
mzazi au mlezi atakae onyesha kikwazo kwa wanafunzi waliofaulu kujiunga na
Kidato cha Kwanza Mwaka 2023 kwa kuwa serikali imeendelea kuboresha Mazingira
ya elimu ndani ya Mkoa wa Katavi.
![]() |
Mwanamvua Mrindoko,Mkuu wa Mkoa wa Katavi akikata utepe kuashiria kuyapokea vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Lyamba Manispaa ya Mpanda (Picha na George Mwigulu) |
Serikali ya Mkoa wa Katavi imesema haita mvumilia mzazi au mlezi atakae onyesha kikwazo kwa wanafunzi waliofaulu kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2023 kwa kuwaserikali imeendelea kuboresha Mazingira ya elimu ndani ya Mkoa wa Katavi.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko wakati akikabidhiwa Madarasa 119 yaliyojengwa kwa fedha zilizotolewa na Rais Dk Samia Suluhu Hassani kwenye hafla iliyofanyika Shule ya Sekondary Lyamba Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Mwanamvua amesema Mkoa wa katavi ulipokea kiasi cha shiligi Bilioni 2 na milioni 380 kwaajili ya ujenzi wa Vyumba vya Mdarasa 119 katika Mkoa wa katavi.
Amesema madarasa hayo yamekamilika na yapo
tayari kuwapokea wanafunzi wa Kidato cha kwanza mwaka 2023 ambapo Halmashauri
ya manispaa ya Mpanda imefakiwa kujenga Vyumba vya Madarasa 51 vyenye thamani ya
Shilingi Bilioni 1.2
Amesema mwaka 2022 wanafunzi 14,904 wamefaulu
kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2023 sawa na 84% kwa Mkoa wa Katavi.
Katika hatua nyingine amefafanua wazazi
serikali haitakuwa na saliamtume kwa mzazi au mlezi atakaeonyesha kikwazo kwa
Mtoto alimefaulu kujiunga Kidato cha kwanza na hatua kali za kisheria kwa
yeyote atakaebainika kukwamisha maendeleo ya watoto kulipoti Shuleni kujiunga
na kidato cha Kwanza.
Mwanamvua amewasihi watendaji wa Serikali
katika mkoa wa katavi Kuendelea kushirikiana katika kumsaidia Rais Dk Samia
Suluhu Hassan Kwenye usimamizi wa fedha za maendeleo zinazo letwa na serikali
ili ziweze kutoa matokea yanayotalajiwa kwa wananchi na serikali kwa ujumla.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa katika Manispaa ya Mpanda,Mkrugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli amesema kuwa Jumla ya wanafunzi 4186 sawa na 86% wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 na vyumba vya Madarasa vimekamilika kwaajili ya kuwapokea wanafunzi hao katika halmsahuri ya manispaa ya Mpanda.
![]() |
Muonekano wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Lyamba Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.(Na George Mwigulu) |
![]() |
Mwonekana wa ndani wa vyumba vya madarasa unaonesha ambao katika shule ya sekondari Mpanda Day Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.(Na George M\wigulu) |
![]() |
Mwonekano wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Lyamba Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi (Picha na George Mwigulu) |
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko (kushoto) akiwa ameketi kwenye moja ya vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Lyamba (Picha na George Mwigulu) |
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika
hafla hiyo akiwemo Said Juma amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuendelea
kuboresha mazingira ya Elimu na kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuja na Mpango wa kujenga vyumba vya
Mdarasa kwaajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.
Helemani Mlowe mkazi wa Manispaa ya Mpanda
akiwa katika hafla hiyo amesema kwa kipindi cha nyuma walikuwa wanahangaika
sana watoto wao kusafiri umbali mlefu kwenda shuleni lakini kwa ujenzi huo wa
Mdarasa utawafanya wanafunzi kuongeza jitihada katika masomo yao.
Kukamilika kwa Ujenzi wa Vyumba vya Mdarasa 119 katika mkoa wa Katavi kutawafanya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka 2023 kuchaguliwa kuanza masomo kwa awamu Moja.