MPIMBWE WAMETEKELEZA KWA WAKATI MAAGIZO YA WAZIRI MKUU

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akipata huduma ya kipimo cha Malaria kutoka kwa Mhudumu wa Afya katika kituo cha afya Majimoto kilichoanza kutoa  huduma 27,December,2022.

Na: OMM-Katavi mkuu.

Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoani Katavi imetekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe,Kassim Majaliwa (mb) la Kituo cha Afya Majimoto kuanza kutoa huduma kwa Wananchi ifikapo 27 Desemba 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumza na baadhi ya wananchi katika kijiji cha Majimoto.

Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoani Katavi imetekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa (mb) la Kituo cha Afya Majimoto kuanza kutoa huduma kwa Wananchi ifikapo 27 Desemba 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko, 29 Desemba, 2022 ametembelea kituo hicho na kushuhudia huduma mbalimbali za Afya zikitolewa na Wataalamu wa Afya Kituoni hapo.

Akizungumza na Wananchi waliofika kupata huduma kituoni hapo Mhe.Mwanamvua ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mpimbwe kwa kutekeleza kwa wakati Maagizo ya Waziri Mkuu ambapo amewataka Wananchi wa Majimoto kuendelea kutunza miundombinu ya Kituo hicho cha kutolea huduma za Afya.


Mhe.Mrindoko amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Wilayani Mlele kuharakisha Ujenzi wa Nyumba za Watumishi kituoni hapo ili waweze kuwa karibu na Mazingira ya kazi ili Wananchi waweze kupatiwa huduma kwa wakati.

Aidha Mrindoko  amesisitiza Wananchi wa Majimoto kutoa ushirikiano kwa Viongozi ikiwa ni pamoja na kutoa Taarifa kwa vyombo husika  iwapo watabaini upotevu wa Dawa na Vifaa tiba.

Mnamo Tarehe 14 Desemba, 2022 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa alifanya ziara Wilayani Mlele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ambapo alitembelea Kituo cha Afya Majimoto na kutoa maagizo ya kituo hicho kuanza kutoa huduma kwa Wananchi ifikapo 27 Desemba 2022.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages