![]() |
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda. |
Na
Walter Mguluchuma,Katavi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imemfikisha Kizimbani Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira wa Manispaa ya Mpanda(MUWASA) Hussein Salumu Nyemba ambae Waziri Mkuu aliiangiza Takukuru kumfanyia uchunguzi.
![]() |
Mkurugenzi wa MUWASA Mpanda - Hussain Nyemba (mbele)akiwa na Justine Wambali kaimu Afiisa Utumishi MUWASA wakifikishwa mahakamani. |
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imemfikisha
Kizimbani Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira wa
Manispaa ya Mpanda(MUWASA) Hussein Salumu
Nyemba ambae Waziri Mkuu
aliiangiza Takukuru kumfanyia uchunguzi
Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stuart Kiondo amewaambia wandishi kuwa mtuhumiwa huyo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda akiwa na mtuhumiwa mwingine KaimuAfisa Utumishi wa( MUWASA ) Justine Wambali mbele ya Hakimu Mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Gaspher Luoga.
![]() |
Mkurugenzi wa MUWASA Mpanda - Hussain Nyemba. |
Watuhumiwahao wamesomewa mashita mawili kila mmoja ambapo shitaka la kwanza wameshitakiwa kwa kosa kutumia vibaya madaraka na shitaka la pili wameshitakiwa kwa kosa la kuisababishia MUWASA hasara ya Tshs 17,817,000. Kinyume na kifungu cha sharia namba 284A(1) sura ya 16 marejeo ya 2022 na kifungu cha sharia Namba 57(1) na 60 (2) cha sharia ya uhujumi uchumi sura namba 200 marejeo yam waka 2022.
Amesemamnamo tarehe 12 mwezi wa 12, 2022 Waziri
Mkuu Kassimu Majaliwa alipokuwa
kwenye ukumbi wa Manispaa ya Mpanda alipokuwa akiongea na watumishi alitowa maelekezo kwa Takukuru kufanya
uchunguzi kwa Hussen Nyemba ambae ni
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na
usafi waMazingirawa Manispaa ya Mpanda (MUWASA)
Katika uchunguzi uliofanywa na Takukuru Mkoa wa Katavi wamewezakubaini kuwa watuhumiwa hao wote wawili wanahusika juu ya tuhuma hizo mbili hari ambayo imewafanya Takukuru kuwafikisha Mahakamani
![]() |
Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi,Stuart Kiondo akitoa taarifa kwa wananhabari ya kufikishwa mahakamani Mkurugenzi wa MUWASA. |
Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stuart Kiondo alieleza kuwamaelekezo ya Waziri Mkuu ilikuwa ni kumfanyia uchunguzi Hussein Nyemba lakini Justine Wambali amejuishwa kwenye kesi hiyo kwa kuwa yeye ni Kaimu Afisa utumishi anawajibika kwani yeye kwa nafasi yake alishindwa kumshauri Mkurugenzi wake na kuajiri watumishi 37 bila kufuata utaratibu na kuisababishia MUWASA kiasi hicho cha fedha .
Amesema
Mkurugenzi huyo amefanikiwa
kutimiza mashariti ya mdhamana
Mahakamani hapo ambapomashariti ya mdhamana kwenye kesi hiyo ilikuwa
kila mtu mmoja awe na mdhamini mwenye
mali isiyo hamishika yenye thamani ya shilingi milioni tano na barua kutoka
kwenye mamlaka zinazotambulika na Serikali .
Hata
hivyo mtuhumiwa Justine Wambali bado anaendelea kutafuta dhamana hadi muda wa
kuhailishwa kwa kesi alikuwa bado haja
timiza mashariti ya mdhamana Mahakamani
hapo .
Kiondo amewaasa watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao kwa sasabu wasipo zingatia maadili upo uwezekano wa kutokea mambo kama hayo pia wakuu wa Taasisisi za umma kwa Mkoa wa Katavi katika utendaji kazi wao wa kila siku wazingatie sharia na maadili na wawe mfano kwa watumishi wao wanao waongoza isitoke jambo kama hili kiongozi wa taasisi kuwa yeye ndie anae husika .
Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi amewaomba wananchi kuendelea kutowa ushirikiano kwa Takukuru ilikuweza kusaidia Mkoa wa Katavi ambao upochini kwa maswala ya Rushwa
Ushirikiano huu pia uwepo kwenye miradi ya Maendeleo miradi ya maendeleo inaletewa fedha nyingi na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan fedha nyingi zinaletwa kwenye mabarabara ,madarasana kwenye sekta nyingine kwa hiyo washirikiane pale pindi wanapoona kuna matatizo kwenye miradi hiyo ili waweze kufatilia kwani miradi hiyo ni mali yao wananchi .