RC MRINDOKO ATOA MASAA 48 MKANDARASI KUFIKISHA VIFAA VYA UJENZI KWENYE MRADI

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko (kwenye picha wa pili kushoto) akiwa anakagua daraja dogo linalotumika kupitishia maji katika bwawa la maji Nsekwa.
(Picha na Walter  Mguluchuma)

Na Walter Mguluchuma,Mlele.

MKUU wa  Mkoa wa Katavi Mwanavua Mrindoko ameiomba  na kuishauri Wizara ya Maji  kupitia  mkataba wa kampuni  ya M/S  HEMATEC INVESTMENT LIMETED  ya Dar es salaam ambayo imeshindwa kukamisha ujenzi wa bwawa la maji la Senkwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele  kwa kipindi cha miaka  mitano sasa  ujenzi linalogharimu  Zaidi ya Shilingi Bilioni 2.

Mkuu wa  Mkoa wa Katavi Mwanavua Mrindoko ameiomba  na kuishauri Wizara ya Maji  kupitia  mkataba wa kampuni  ya M/S  HEMATEC INVESTMENT LIMETED  ya Dar es salaam ambayo imeshindwa kukamisha ujenzi wa bwawa la maji la Senkwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele  kwa kipindi cha miaka  mitano sasa  ujenzi linalogharimu  Zaidi ya Shilingi Bilioni 2.8.

Pia ametowa masaa 48 kwa mkandarasi huyo kuwa amefikisha  vifaa vya kujengea maradi huu na kama hata  hata tekeleza agizo hilo Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mlele (OCD) ameagizwa kumsaka popote pale alipo nakumweka ndani .

Mkuu huyo wa Mkoa alitowa ombi hilo mara baada ya kukagua mradi huo na kutoridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao utelelezwaji wake bado bado sio wa kuridhishwa  licha ya kuanza kutekelezwa miaka  mitano iliyo pita .

Amesisitiza kuwa  Serikali haiwezi  kuona wananchi wake  wanateseka kwa ajiri ya uzembe wa mkandarasi wakati fedha Zaidi ya bilioni 1.9 zimesha tolewa lakini mradi huo bado ujenzi wake ni wa kususua

Amebainisha  kuwa yeye kama mkuu wa mkoa amefika kwenye eneo hilo la Mradi mara nne lakini haoni maendeleo yeyote ya Mradi huo na wameshatoa ushauri kama mkoa kwa Ruwasa Makao makuu mkoa na wilaya lakini hakuna zozote zilizochukuliwa mpaka sasa

Ameiomba Wizara ya Maji kuchukua hatua za Kimkataba kwa Mkandarasi huyo kwani hafai kutekeleza tena Mradi huo kwa uzembe unaoonekana kwa kutokamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Mwakilishi wa Meneja  wa Ruwasa Halmashauri ya wilaya ya Mlele Mhandisi Madaha Majagi alisema Mradi huo unathamani ya shilingi Bilioni 2,895,334 494 .00,00 ambapo ikiwa ni gharama za ujenzi wa Tuta na utoro wa Maji, na Bilika la kunyweshea Mifugo ambapo mpaka sasa kiasi cha shilingi Bilioni 1,924,665,566.00,00 ameshalipwa Mkandarasi.

Mradi huo ulianza kutekelezwa 3/8/2018 ambapo ulitakiwa kukamilika 3/8/2019 Mradi huo unaendelea na haujaanza kutoa huduma kwa wananchi.

Mradi huo wa Maji unatalajiakunufaisha vijiji vipatavyo 16 katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele ujenzi huo wa Bwawa na ujenzi wa Daraja Dogo utekelezaji wake umechelewa kwa sababu ya Kasi ndogo ya utekelezaji kutoka kwa Mkandarasi hivyo ameongezewa muda hadi mwezi huu wa Desemba 2022.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages