WAKANDARASI WAZAWA WA KATAVI WAHIMIZWA KUMILIKI MITAMBO MIKUBWA.

 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi ,Mwanamvua Mrindoko (wa pili kutoka kushoto kwenye picha)akiwa kwenye eneo la mradi wa barabara Inyonga kuelekea Mapili iliyojengwa na lami na TANROAD Mkoa wa Katavi. (Picha na Walter Mguluchuma)

Na Walter Mguluchuma,Mlele.

Wakala wa Tanzania Tanroads Mkoa wa katavi wataendelea  Kuhamasisha Wakandarasi wa  Mkoa wa Katavi waweze kumiliki Mitambo Mikubwa ili kuondokana na changamoto iliyopo sasa ya wakandarasi wa mkoa wa Katavi kukodi Mitambo kwenda Sehemu Nyingine pindi wanapokuwa wamepewa kazi ya Matengenezo ya Barabara.

Wakala wa Tanzania Tanroads Mkoa wa katavi wataendelea  Kuhamasisha Wakandarasi wa  Mkoa wa Katavi waweze kumiliki Mitambo Mikubwa ili kuondokana na changamoto iliyopo sasa ya wakandarasi wa mkoa wa Katavi kukodi Mitambo kwenda Sehemu Nyingine pindi wanapokuwa wamepewa kazi ya Matengenezo ya Barabara.

Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mhandisi Emili Zengo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya ujenzi wa Barabara zinazo tekelezwa katika Wilaya ya Mlele mbele mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alipokuwa na ziara ya kukagua miradi ya Barabara inayotekelezwa katika wilaya ya Mlele.

Amesema wakanadarasi wa Mkoa wa katavi wanakabiliwa na Changamoto ya ukosefu wa mitambo Mikubwa inayo wawezesha kufanyia kazi za Matengenezo ya Barabara ambapo mitambo mingi hutegemea kukodi hali inayo pelekea miongoni mwao kuchelewa kutekeleza miradi hiyo kwa wakati.

Hivyo Tanroads wanaendelea kuhamasisha wakanadarasi wazawa waweze  kumiliki mitambo mikubwa na wamiliki wengine wa Mitambo ambao wapo nje na mkoa wa katavi wahamishie mitambo hiyo mkoa wa katavi ili ujenzi wa Barabara ziwe zinakamilika kwa muda uliopagwa.

Wataendelea kusimamia matengenezo ya Barabara kuu na Barabara za mikoa pamoja na kuhusisha barabara zao zinazopita kwenye Miji Midogo kutoka kiwango cha Chanagalawe kuwa kiwango cha lami kwa lengo la kupendezesha miji na kuchochea maendeleo kwa wananchi.

Mhandisi Zengo amebainisha kuwa kati yam waka wa fedha 2017/18 hadi 2021/22 Tanroads wamejenga kiwango cha Lami kilomita 15. 9 katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele.

Na katika mwaka huu  wa fedha 2022/23 wamepanga kujenga Barabara kilomita 2 za kiwango cha Lami katika Mji wa Ilunde na mita 400 katika hospital ya wilaya ya Mlele.

Sambamba na ujenzi huo wataweka Taa za barabarani katika mji wa Inyonga na Mji wa Mapili lengo ikiwa ni kuwaboleshea watanzania Mazingira bora ya uchukuzi wa kimiundimbinu.

Zengo alisema hadi November 30 mwaka 2022 kati ya Miradi nane inayotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Mlele Miradi Saba imeshapata Msamaha wa ongezeko la Samani ujenzi katika miradi hiyo upo katika hatua mbalimbali ambapo miradi Mingi ipo kwenye hatua ya Kuleta vifaa na miradi michache ambayo inahitaji Mitambo mikubwa.

Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Mlele kuhakikisha wanazingatia mambo yote yanayokatazwa kwenye Barabara.

Mwakilishi wa Meneja wa TANROAD Mkoa wa Katavi,Mhandisi Emily Zengo (wa kwanza kushoto kwenye picha) akitoa taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko (wa kwanza kulia)alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi barabara unaotekelezwa na TNAROAD katika halmashauri ya wilaya ya Mlele Mkoani hapo.
(Picha na Walter Mguluchuma)

Kwani Serikali inafanya kazi kubwa yakubolesha miundombinu Mbalimbali hivyo wananchi wanapaswa kutambua kuwa miradi hiyo inamanufaa kwa wananchi.

Amewaonya wanachi watakao diliki kujihusisha na uondoaji wa Aalama za barabarani ikiwemo Solar za taa za barabarani,alamaza za barabarani pamoja na kulima kando ya barabara serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa wale watakao jihusisha na vitendo hivyo.

 Mkazi wa kijiji cha Mapili Nyanga Mwita amesema toka wamewekewa lami kijijini hapo kutokea katika mji wa Inyonga hali ya usafirishaji wa Mazao umeshuka tofauti na hapo awali ambapo Gunia moja la kilo 100 kupeleka katika mji wa Inyonga walikuwa wanatozwa kiasi cha shilingi Elfu 5000 huku kwa sasa wakisafirisha Gunia moja la kilo 100 kwenda Mji wa Inyonga kwa shilingi 1500.

 Asha Fadhili,Mkazi mwingine wa  kijiji hicho ameeleza kuwa walikuwa na changamoto ua usafiri kwa kutumia Gharama kubwa ya usafiri kutoka kijijini hapo hadi katika mji wa Inyonga walikuwa wanatozwa kaisi cha shilingi elfu 10000 kwa Boda boda huku sasa hivi wakitozwa kiasi cha shilingi elfu 2000.

Ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kwajali wanachi n ahata wa pembezoni kwa kuwaboreshea miundombinu mbalimbali ya barabara, Maji,Afya na Elimu kwa kiwango cha kulidhisha.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages