BAKWATA KATAVI JAMII IWE NA MOYO WA KUSAIDIA WATOTO

Shekhe Mkuu wa Bakwata  Mkoa wa Katavi Mashaka Nassoro Kakulukulu akikabidhi sale za shule kwa watoto wanaishi katika mazingira magumu wilaya ya Mpanda katika zoezi lililofanyika kwenye Viunga vya Msikiti mkuu wa Ijumaa Mpanda Katavi. [Picha na Goerge Mwigulu]

Na Paul Mathias-Mpanda.
Jamii imeaswa kuendelea kusaidia Makundi ya watoto yenye Uhitaji maalumu  katika jamii ili kusaidia kuzifikia ndoto zao za kimaisha kwa kupitia Elimu.

Shekhe Mkuu wa mkoa wa Katavi Mashaka Kakulukulu [watano kushoto]akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bakwata mkoa wa katavi na watoto waliopatiwa masaada wa sale za shule[Picha na George Mwigulu] 

Wito huo umetolewa na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mashaka Nassoro Kakululukulu wakati akikabidhi sale za Shule kwa watoto 29 wanaoishi katika mazingira magumu wilaya ya Mpanda.

Kakulukulu amesema wanaungana na Serikali katika kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu na kwakuwa serikali imesha fanya kazi nzuri kwenye ujenzi wa miundo ya madarasa katika kila eneo.

Ameeleza kuwa wao kama viongozi wa dini katika mchango wa kuiunga mkono serikali wanaowajibu wa kuhakikisha watoto wanaenda kusoma wakiwa kwenye mazingira mazuri ikiwa nipamoja kupata vitendea kazi zikiwemo sale za shule.

Amesema “leo tupo hapa kwaajili ya kutoa sale za shule kwa watoto wa kike nawakiume kwa kuwapatia Shati na sketi na Kaptula kwakuzingatia kuwa hivi karibuni shule zinafunguliwa na tuwaone watoto hawa kama watoto wetu.”

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa jamii na wadau mbalimbali kwa kuendelea kuwasaidia watoto wanaishi katika mazingira magumu katika suala la elimu kwakuwa elimu ni taa kwaajili ya maisha yao ya baadae.

Shekhe Mkuu wa Bakwata  Mkoa wa Katavi Mashaka Nassoro Kakulukulu akikabidhi sale za shule kwa watoto wanaishi katika mazingira magumu wilaya ya Mpanda katika zoezi lililofanyika kwenye Viunga vya Msikiti mkuu wa Ijumaa Mpanda Katavi. [Picha na Goerge Mwigulu]

Hidaya Joseph mmoja wa wazazi anaoishi na watoto wawili ambao wamenufaika na msaada huo amesema anawashukuru wote waliotoa sadaka hiyo ya mavazi.

Amewashukuru viongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mpanda na wote waliochangia na hawana cha kuwalipa mwenyezi Mungu atawalipa kwa kile walichotoa kwa watoto hao.

Hidaya amebainisha kuwa kwa mara kadhaa amekuwa akiwalea watoto hao kwa yeye kujishughulisha katika biashara ndogondogo kwa msaada huo umempunguzia kidogo changamoto hiyo kwa watoto hao.

“Kabla ya kupata huu msaada ninapambana mimi Bibi yao nahangaika biashara nakuhakisha watoto wanakwenda shule kwa sasa namushukuru mwenyezi Mungu kila kitu kitaenda sawa alisisitiza”

Asha kassimu Mwanafunzi wa shule ya msingi nyerere nashukuru sana kwa msaada waliotupatia mungu awabariki sana.

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages