MVUA KUBWA YALETA TAFURANI MPANDA


Hapa ni sehemu ya makazi yal mtaa wa Uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpanda Mkoawa Katavi yakiwa na mafuriko baada ya mvua kuwa kunyesha.
 

Na Walter Mguluchuma,Katavi

Mvua kubwa imenyesha na kuambatana na upepo mkali pamoja na mawe imesababisha barabara ya kutoka Kata ya Majengo inayounganisha na Kata ya Uwanja wa ndege imesababisha barabara ya kwenda uwanja wa ndege wa mpanda na kushindwa kupitika huku ikiharibu nyumba tatu kwa maji kuingia ndani ya nyumba hizo.

Mvua kubwa imenyesha na kuambatana na upepo mkali pamoja na mawe imesababisha barabara ya kutoka Kata ya Majengo inayounganisha na Kata ya Uwanja wa ndege imesababisha barabara ya kwenda uwanja wa ndege wa mpanda na kushindwa kupitika huku ikiharibu nyumba tatu kwa maji kuingia ndani ya nyumba hizo.

Kati ya nyumba hizo tatu zilizojaa maji nyumba mbili wamefanikiwa kutowa baadhi ya vitu huku nyumba moja ikiwa imeshindikana kutowa kitu hata kimoja kufuatia nyumba hiyo kujaa maji mengi sana .

Afisa Tarafa wa Tarafa ya Kashauli Bonimpaye Nkoronko amesema kuwa kimsingi barabara hiyo ni kiunganishi kati ya Kata ya Majengo na Kata ya Uwanja barabara hiyo ndio inayoelekea katika uwanja wa Ndege wa Mpanda hari hiyo pamoja na kutokea hakuna maafa ya kifo chochote ambacho kimeweza kutokea kutokana na mafuriko hayo ya maji ya mvua .

Amesema baada ya tukio hilo wameisha wasiliana na wakala wa Barabara Tanzania TANROADS ambao wameweza kufika kwenye eneo hilo na kuwasiliana na Jeshi la Zima Moto na Uokoaji na Polisi ambao nao wamefika kwenye eneo kwa ajiri ya kuhakikisha usalama wa Wananchi wa maeneo hayo .

Amewaomba wananchi wawe watulivu kwani maji hayo yanapungua kwa kasi kubwa hivyo muda si mrefu barabara hiyo itapita kwani hakuna sehemu ambayo barabara ilipo aribika na watu wataendelea na shughuli zao kama kawaida .

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mwandisi Martini Mwakabende amesema mchana wa leo kuna mvua kubwa ambayo imenyesha na katika barabara hiyo hakuna uharibifu wowote ule wa barabara ulitokea na wanaendelea kusubiria maji yapungue ndio waweze kujua nini cha kufanya .

Amewahakikishia wananchi kuwa pamoja na hari hiyo bado kuna barabara mbadala ya kupitia ya kiwango cha lami inayotoka Mpanda mjini kuelekea Mkoani Tabora ambayo inawafikisha watu hadi kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda na kwenye makazi ya wananchi wa uwanja wa ndege

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages