Na Paul mathias –Katavi
Chama cha Mapinduzi CCM katika mkoa wa Katavi kimempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu Hassani Kwa kitendo chake cha Kuondoa zuio la Kufanyika kwa mikutano ya kisiasa alilolitoa mnamo January 3,2023 Ikulu Jijini Dar es Salamu wakati akiongea na viongozi wa vyama vya siasa.
Akisoma Tamko hilo la pongezi kwa niaba ya wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM kwenye kongamano lililofanyika katika ukumbi wa Mapnada social hall Manispaa ya Mpanda Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Katavi amesema .
“Kwaniaba ya chama cha Mapinduzi mkoa wa Katavi na wanachama wa chama cha mapinduzi mkoa wa Katavi Tunampongeza na kumuunga Mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kauli yake alioitoa Juzi 3,January 2023 ya kutengua zuio la kufanyika kwa Mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa, mkoa wa Katavi tunamuungamkono tupo pamoja nae katika kukuza Democrasia na kujenga umoja wa kitaifa”
Kimanta
amesema Rais Dkt samia Suluhu Hassan
amekuwa mstari wa mbele kuionyesha Dunia kuwa watanzania tutaendelea kuwa
wamoja na kuwa watulivu na kuendesha siasa zetu kwa amani ili nchizingine ziige
mfano kutoka Tanzania
Ameeleza
kuondolewa kwa hilo kusiwe chanzo cha vulugu na kuvunjiana heshima na
kutukanana balikuewepo na siasa za kustahimiliana nakusisitiza na chama cha mapinduzi kitanya mikutano yake
kwa amani na utulivu
Ametoa wito
kwa vyama vingine vya siasa kufanya mikutano yao kwa amani na utulivu kwa
kuongozwa na hoja zenye kujenga na kuisadia serikali ya chama cha mapinduzi ili
kutatua changamoto na kero zinazo wagusa wananchi moja kwa moja
Mkuu wa mkoa
wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya
chama chama cha Mapinduzi katika kongamano hilo amesema serikali imefanya mambo
mengi ya maendelea katika sekta ya barabara kwa kuasaidia mkoa wa katavi
kuunganishwa na mkoa wa Tabora kwa kiwango lami hali ianayopelekea kuchochea
maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi
Katika sekta
ya Maji Mrindoko ameeleza kumekuwa na uboreshaji wa upatikanaji wa maji mijini
na vijijini kwa kiwango kinachoridhisha kwa msukumo wa serikali ya wamu ya Sita
ya Dkt Samia suluhu Hassan kuendelea kuleta Fedha kwaajili ya utekelezaji wa
miundombinu hiyo
Awali akitoa
neno kwa niaba ya Wenyeviti wa
halamsahauri kwenye kongamano hilo Mstahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary
Summry amesema anatoa shukurani kwa Rais Dk samia suluhu Hassan kwa kuendelea
kuleta fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri
Moja ya Bango lenye ujumbe kwa Rais Dkt Samia suluhu katika kongamano la kumpongeza kwa kutengua zuio la mikutano ya hadhara |
Nae mbunge wa Viti maalumu mkoa wa katavi Martha Maliki amesema watakenda kuyasema yaleyote yananayofanywa na Serikali ya Dkt Samia suluhu Hassan kwa wanachi kwakuwa yanajipambanua kwa macho na kila mtu anayaona.