Na Paul Mathias-Mpanda
Balaza la Madiwani katika halamsahauri ya Manispaa ya Mpanda
Mkoa wa Katavi limepitisha kiasi cha shilingi Bilion 26.4 kwaajili ya kukusanya
na kupokea kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wakiwa katika kikao maalumu cha kupitia na kupanga Rasimu ya Bajeti ya halamsahauri hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 [PICHA na Paul Mathia]
Balaza la Madiwani katika halamsahauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi limepitisha kiasi cha shilingi Bilion 26.4 kwaajili ya kukusanya na kupokea kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024.
Kila muhama amesema katika Rasimu hiyo ya Mpango wa Bajeti
Matumizi ya Kwaida Bilioni 17 huku Bilioni 9 zikitengwa kwaajili ya Miradi ya
maendeleo katika Bajeti hiyo kupitia Mapato yake ya ndani halmashari ya
Manispaa ya Mpanda imetenga Milioni 400 kwaajili ya Ujenzi wa Maboma 100 ya
Mdarasa.
Pamoja na hayo halmashauri hiyo imetenga kiasi cha milioni 70 kwaajili ya Kuwalipa Wakandarasi mbalmbali madeni yao wanayoidai halmashauri hiyo halikadhalika kupitia mapato ya ndani zikitengwa Milioni 100 kwaajili ya kufungua Barabara kwenye Maeneo yaliyopimwa.
Msitahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry amesema
Bajeti hiyo itakwenda kutekeleza Shughuli mbalimbali za Maendeleo ya wananchi
wa Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda na wao kama balaza la Madiwani wametimiza
takwa hilo la kisheria la kupitisha rasimu hiyo ya bajeti.
“jumla kuu sasa inafanya jumla ya Bajeti ya jumla kwa maana ya
Mapato ya ndani na mapato kutoka serikali kuu wafadhili na Mishara kuwa jumla
ya shilingi bilioni 26.4 hivyo ndugu waandishi wa habari bajeti yetu imepita
kama nilivyo eleza na itaendelea kwenye hatua zingine tukitoka kwenye baraza
tunakwenda DCC na RCC kwaaajili ya kushauriwa”amesema Haidary
Wiliamu Mbogo Diwani wa Kata ya Majengo halmshauri ya Manispaa
ya Mpanda katika mchango wake kuhusu Bajeti hiyo ameiomba halmashauri kuendelea
kutenga fedha katika eneo la kilimo cha Korosho kama zao la kimukakati ikiwa
nisehemu ya kuwekeza kilimo hicho hasa kwa vijana.Diwani wa Kata ya Kawajense Uwezo Bachu akichangia hoja kwenye kikao maalumu cha kupanga na kupitisha Bajeti ya halmashauri ya Manispaa ya Mpanda [Picha na Paul Mathias]
Ukiangalia kwenye Bajeti hii naona imetengwa milioni 4 kwaajili
ya hamasa kwa zao la Korosho fedha hii ahaitoshi kwa kilimo hiki kuweka hamasa
kwenye zao la korosho
“kuna msemo wa kikonongo wengine wanakula wengine wanatimaza kwa
macho hivyo tusije kuwa watazamaji wenzetu wa mikoa ya kusini wakiendelea
kuvuana Mabilioni ya fedha kupitia kilimo hiki cha korosho”alihoji Mbogo.
Kwa upnde wake Uwezo Bachu Diwani wa kata ya Kawajense Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda amehoji mkataba wa Mradi wa kusindika nafaka katika eneo la kata ya Misunkumilo kutofanya kazi huku halmashauri ikiendelea kupoteza mapato.
Wiliamu Mbogo Diwani wa kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda akichangia jambo katika Kikao maalumu cha kupanga na kupitisha Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda [Picha na Paul Mathias] |
Bachu ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa Elmu Bure kwa
ngazi ya Shule ya Msingi Hadi Sekondari hali ambayo imewapa unafuu wanachi
wenye watoto kuongeza hamasa ya kuwapeleka watoto wao shule.
Katibu tawala Mkoa wa Katavi Hassan Abas Rugwa akiwa Mgeni
mwalikwa katika balaza hilo ameikumbusha halmashauri hiyo kuwa makini katika
mikataba wanayo ingia hasa katika maeneo ya vibanda kwenda na wakati uliopo ili
kuepuka kupoteza mapato ya halmashari.
Rugwa ameshauri madiwani kwenda kusimamia usawa wa Mgawanyo wa fedha za halmashari kupitia mikopo ya vijana wanawake na wenye ulemavu kuzingatia miazania na kanuni zilizowekwa kwani “kunafedha zinaoneka lakini kulipwa kwake kumekuwa na changamoto hasa hizi zinatotolewa na halmashauri”.
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com