MWANA KIJIJI MBARONI KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO

 

Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi Ali Makame Hamad akizungumnza na waandishi wa Habari wa mkoa wa Katavi ofisini kwake [PICHA na Paul Mathias]

Mwanakijiji wa Kitongoji  cha  Ipota  Kijiji cha Ikuba  Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi  Shija  Ntumbili  anashikiliwa na Jeshi la Polisi  kwa   tuhuma za kukamatwa  na meno ya Tembo mawili .

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame amewaambia Wandishi wa Habari kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa kufutia msako makali uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Askari wa Tanapa .

Amesema kabla ya mtuhumiwa huyo kukamatwa jeshi la polisi walikuwa wamepata taarifa juu ya mtuhumiwa huyo kujihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo .

Baada ya kuwa wamepata taarifa hizo ndipo jeshi la polisi kwa kushirikiana na Askari wa Tanapa  walianza kufanya msako   mkali .

Kamanda Ali Hamad Makame ameeleza kuwa kufuatia msako huu ndipo walipoweza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa  ameyahifadhi meno hayo ya tembo mawili  akiwa ameyahifadhi ndani ya nyumba yake .

Amebainisha kuwa taratibu zinaendelee  za kwenye idara husika ili kuweza kujua mano hayo mawili yanathamani ya kiasi gani .

Amesema mtuhumiwa bado anaendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi na anatarajiwa kufikishwa wakati wowote Mahakamani ili  akajibu tuhuma zinazo mkabili.

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages