WANAFUNZI 24,000 WA SHULE ZA MSINGI MKOA WA RUKWA HAWAJUI KUSOMA.

 

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Rashidi Mtachatta  [aliekaa katikati] akiwa katika
picha ya Pamoja na Waandishi wa Habari Mkoa wa Rukwa kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari kuhusu Mradi wa Shule.

Na Israel Mwaisaka,Nkasi-Rukwa.

Mkoa wa Rukwa una wanafunzi wa shule za msingi wapatao 24,000 hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Rashid Mchatta akitoa tathimini ya Masuala ya Elimu mkoa wa Rukwa wakati wa Mafunzo ya utekelezaji wa Mradi wa Shule Bora katika Mkoa wa Rukwa.
Mkoa wa Rukwa una wanafunzi wa shule za msingi wapatao 24,000 hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Ofisa elimu wa mkoa huo, Samson Hango aliyabainisha hayo jana wilayani Nkasi  mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa,   Rashid wakati akifungua mafunzo ya y Program ya Shule Bora  ya siku moja kwa waandishi wa habari, na Maofisa Ellimu Msingi kwa lengo la kuwajengea uwezo wafahamu kuhusu mradi wa Shule Bora unaotekelezwa mkoani humo.

Amesema kuwa kutokana na utafiti uliofanyika mwezi Desemba mwaka 2022  ulibaini kuwa katika mkoa  wa Rukwa kuna wanafunzi 24,000 Kati ya 300,000 wa shule za msingi ambao hawajui kabisa kusoma, kuandika na kuhesabu.

"kutokana na utafiti uliofanyika Desemba mwaka jana ilibainika kuwa Kuna wanafunzi 24,000 Kati ya zaidi ya wanafunzi 300,000 wa shule za msingi ambao hawajui kabisa 'K'  tatu, hali ambayo inatulazimu tupambane ili wanafunzi hao wazijue hizo K tatu ambao ndio msingi wa Elimu" alisema. 

Akifungua mafunzo hayo Katibu tawala wa mkoa wa Rukwa, Mchata alisema kuwa vyombo vya habari Mkoani humo bado havijaripoti vya kutosha kuhusu changamoto zilizopo katika sekta ya elimu. 

Alisema kuwa sekta hiyo bado haijafanya vizuri Sana hivyo ni wajibu wa wanahabari kuibua changamoto zinazo ikabili ili zitafutiwe ufumbuzi hali ambayo itasaidia kukuza kiwango cha ufaulu Mkoani humo.

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.co.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages