RC MRINDOKO TUNAAKIBA YA MADARASA KWA AJILI YA WANAFUNZI.


Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa huo Idd Kimanta (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,Jamila Yusuph (kushoto) wakiwa kwenye shule ya Sekondari Kawalyowa wakati wa Ukaguzi na upandaji miti.

Na George Mwigulu,Mpanda.

Idadi ya wingi wa vyumba vya madarasa hadi kupelekea nyongeza ya madarasa ya akiba katika Mkoa wa Katavi umewezesha wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 kuchaguliwa kwa awamu ya kwanza ambapo wazazi na walezi wa watoto wametakiwa kuhakikisha ifikapo 9, January shule zinapofunguliwa wanafunzi wanafika shule bila kukosa.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko (ameshika mti) akipanda mti katika shule Kawalyowa akiwa ni juhudi za uhifadhi wa mazingira katika shule hiyo.

Idadi ya wingi wa vyumba vya madarasa hadi kupelekea nyongeza ya madarasa ya akiba katika Mkoa wa Katavi umewezesha wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 kuchaguliwa kwa awamu ya kwanza ambapo wazazi na walezi wa watoto wametakiwa kuhakikisha ifikapo 9, January shule zinapofunguliwa wanafunzi wanafika shule bila kukosa.

Mwanamvua Mrindoko,Mkuu wa Mkoa wa Katavi amesema hayo mbele ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa huo,Idd Kimanta wakati kupanda miti na kukagua shule ya sekondari   Kawalyowa  Manispaa ya Mpanda ambapo ameelezea nia njema ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuboresha zaidi sekta ya elimu.

Mkuu wa Mkoa huyo ameweka wazi kuwa mchanganyiko wa ujenzi wa shule sita mpya katika halmashauri za mkoa huo pamoja na vyumba vya madarasa 119 yaliyojengwa kwa fedha maarufu kwa jina la “fuko la Samia”  imefanya kuwa na jumla ya vyumba vya madarasa 355 yanauwezo wa kupokea wanafunzi wapya.

“…jumla ya vyumba vya madarasa 355 yatapokea wanafunzi wapya lakini kwa idadi ya wanafunzi waliofaulu  ni 14,904 ikiwa mahitaji yao ni takribani vyumba vya madarasa 299 utaona kuwa tunanyongeza ya madarasa mengi yaliyo baki hata kama wanafunzi wote waliofanya mtihani wangefaulu madarasa hayo yangewatosha wakiwa wamekaa kwenye madarasa mazuri na madawati” amesisitiza Mrindoko.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda,Sophia Kumbuli akitoa maelezo juu ya ujenzi wa mradi wa shule ya sekondari Kawalyowa 

Ni shule ya sekondari Kawalyowa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ambayo imeaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza.

Majengo haya ni mwonekano wa nje wa baadhi ya vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Kawalyowa iliyopo manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Majengo haya ni mwonekano wa nje wa baadhi ya vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Kawalyowa iliyopo manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Mrindoko ameeleza kuwa katika halmashauri nne za Mkoa wa Katavi zimepata shule moja moja na halmshauri ya manispaa ya Mpanda imepata shule mbili zote zikiwa zililetewa fedha Mil 470 kwa ajili ya ujenzi ambapo tayari zimekamilika kujengwa na ziko tayaru kutumika.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Katavi amemhakikishia Mwenyekiti wa CCM Mkoa kuwa ilani ya chama hicho inaendelea kutekelezwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa fedha  kwenye sekta ya elimu hasa ya sekondari.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi,Idd Kimanta akipanda mti katika shule ya sekondary Kawalyowa Manispaa ya Mpanda ikiwa ni sehemu ya kuonesha ishara ya utunzaji wa mazingira (Picha na Paul Mathias)

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi,Matha Maliki akipanda mtu katika shule ya sekondari Kawalyowa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tangantika,Yasin Kiberiti  akipanda mtu katika shule ya Sekondary Kawalyowa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Iddi Kimata amesema kuwa chama kimeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya chama hichi kupitia ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa Mkoani Katavi.

Aidha akiwa katika shule ya sekondari Kawalyowa ametoa nasaha kwa wanafunzi waliochanguliwa kujiunga na masomo katika shule hiyo kusoma kwa bidii na hatimaye kuweza kuzifikia ndoto zao za kimaisha kupiti elimu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Sophia Kumbuli anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo kama Manispaa wametekeleza jukumu hilo kikamilifu.

Kumbuli amesisitiza kuwa fedha za mapato ya  ndani wametegea Mil 104  na zimepata ridhaa kwa ajili ya kukamilishaji wa milango na madirisha ambapo kwa bahati nzuri ndani ya bajeti yao walikuwa na Mil 20 tayari zimetumika kwa ajili ya utengenezaji wa madawati .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages