CCM : MPANDA YAPANDA MITI 2000 KUELEKEA MIAKA 46

 

Ofisi kuu ya chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi[ Picha na Paul mathias]
Na Paul Mathias.

Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda kimesema kuwa kitafanya kumbukizi ya kuzaliwa kwa chama hicho kwa kufanya matendo ya kijamii na kutembelea Miradi ya maendeleo.

Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda Sadiki Kibwana Kadulo  akizungumnza na Katavi Press blog ofisini kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi CCM[Picha na Paul Mathias]

Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda Sadiki Kibwana Kadulo ameseya sema hayo katika mahojiano maaalumu na chombo hiki kuelekea Maazimisho ya Miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi mnamo 5/2/1977.

Amebainisha kuwa katika kuelekea siku hiyo tayari kazi za kijamii zimeanza kufanyika kwa kufanya matendo mbalimbali ya kijamii  Kupitia Jumuiya za chama ikiwemo Kupanda miti ikiwa nisehemu ya kuhamasisha utunzaji wa Mazingira.

“Sisi sasa hivi hapa CCM Wilaya ya Mpanda tumesha panda miti katika Kata zetu na katika majengo ya serikali na majengo ya taasisi binafsi tumepanda miti 2000 mpaka sasa hii ni kuonesha kwamba sisi tumejipanga katika kuhakikisha kwamba Mpanda niyakijani hayo yote tunayafanya katika bidiiza kuhakikisha kwamba chamakinaendelea kuwa hudumia wananchi”amesema kadulo

Amesema kuwa chama hicho wilaya ya Mpanda Tarehe 1na 3/2/2023 watatembelea Kituo cha afya Ilembo kuwajulia hali wagojwa kufanya usafi na kupanda miti halikadhalika watatembelea kituo cha afya kakese kufanya tendo la huruma pamoja na kutembelea mradi wa ujenzi wa ofisi ya chama cha Mapinduzi kata ya kakese.

Jenifer Bakila mwana chama wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda alipokuwa anatoa maoni yake kuelekea miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi CCM [Picha na Paul Mathias]

‘’sisi tarehe 1/2/2023 tutakwenda kituo cha Afya Ilembo tutafanya tendo la Huruma tutafanya usafi lakini tutapanda miti na kuwaona wagojwa na tutatoa zawadi za pole kwa wagojwa hao kwakile tutakuwa nacho,tutakwenda hapo ilembo kwenye eneo letu la CCM kunanyumba ya Mtumishi pale ambayo tumejenga ya kisasa kabisa ambayo inagharimu karibu milioni 100  tutapanda miti na kufanya usafi baada ya hapo tutakwenda kakesse”

Kuhusu kilimo kadulo amesema serikali ya Dk Samia suluhu Hassani imeboresha mazingira ya kilimo kwa wakulima wakubwa na wadogo katika wilaya ya Mpanda kwa kukopeshwa zana za kilimo hasa Matrekita pamoja na mpango wa utoaji wa Mbolea ya luzuku kwa wakulima katika wilaya ya Mpanda.

Jenifer Bakila Mwanachama wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mpanda anasema maazimisho hayo yatakuwa chachu ya kuendelea kuongeza wanachama katika chama cha mapinduzi na kuongeza vijana wengi katika chama hicho ili kukisaidia chama kwa kuwaletea wananchi maendeleo.

Hatuhimana James Mwanachama wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda amesema maazimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi CCM ni sehemu mhimu ya kupima utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi CCM[ Picha na Paul Mathias]
“kwanza kabisa maazimisho haya yanatija kwa kuongeza wanachama katika chama chetu hasa vijana lakini pia chama cha Mapinduzi kimetuletea maendeleo makubwa sana kimetutengenezea barabara watoto wamepata madarasa na Madawati na hospitali tumepata mambo mengi tumefanyiwa na chjama cha Mapinduzi”

Kwa upande wake Hatuhimana James mwanachama wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Mpanda anaeleza kuwa maadhimisho hayo kufanyika itasaidia kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi katika maeneo ya Miradi.

“Katika kujenga chama tunajitengenezea Mazingira mazuri katika ile hali ya kutekeleza ilani ya chama pia lakini pia watu wataendelea kujua umuhimu wa chama katika utekezaji wa ilani”

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages