Na Paul Mthias- Katavi
Serikali katika mkoa wa Katavi Kupitia ofisi ya Mlajisi imeanza
Mkakati wa Kuhakikisha Vyama vya Ushirika vina kuwa na uwezo wa kuandaa taarifa
za fedha na kumbukumbu za fedha ili kuepuka Kupata hati chafu au hati zenye
mashaka kwa wakaguzi wa Nje.
Serikali katika mkoa wa Katavi Kupitia ofisi ya Mlajisi imeanza Mkakati wa Kuhakikisha Vyama vya Ushirika vina kuwa na uwezo wa kuandaa taarifa za fedha na kumbukumbu za fedha ili kuepuka Kupata hati chafu au hati zenye mashaka kwa wakaguzi wa Nje.Mlajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Katavi Peter Nyakunga akiwahutubia washiriki wa mafunzo kutoka vyama mbalimbali vya ushirika Mkoa wa Katavi[Picha na paul mathias]
Peter Nyakunga Mlajisi
Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Katavi amesema wamefanya mafunzo ya Siku
Sita na watendaji wa vyama vya Msingi na wajumbe wa Bodi kwa lengo la
kuwajengea uwezo juu ya namna bora ya kuandaa taarifa za fedha na kumbukumbu
zake.
‘’nyakunga anasema katika mkoa wetu wa Katavi tulipta taarifa
kutoka kwa mkaguzi wa nje vyama vilivyokaguliwa kwa msimu wa Mwaka 2021 katika
vyama 34 vilivyokaguliwa hakuna chama hata kimoja ambacho kimeweza kupata hati
Safi vyama vyetu vyote vyama 14 vilipata hati yenye shaka tuna vyama 12
vilipata hati isiyo lidhisha tuna vyama 8vilipata hati mbaya ama hati chafu”
Amesema kwa kuliona hilo imewalazimu kufanya mafunzo hayo kwa
vyama vyote 47 vilivyopo mkoa wa Katavi kwa lengo la kuhakikisha vyama hivyo
vya ushirika vianaondokakana na hali hiyo ya kuwa na hati chafu au mbaya kwenye
hoja za ukaguzi wa nje.
“tuliona kuna shida katika utunzaji wa kumbukumbu za chama sasa
tukasema mafunzo haya tuite watalamu kuja kutusaidia kutufundisha tuweze
kuandika ilea miamala yetu kila siku iweze kukaa vizuri tutunze kumbukumbu zetu
za uhasibu vizuri ili tutakapo kwenda kupeleka hesabu zetu kwa mkaguzi hizi
hati mbaya tuepukane nazo”
Kwa kipindi hicho cha siku sita wameweza kupitishana na kukumbushana
juu ya Misingi ya uendeshaji wa vyama vya ushirika kwa kuzingatia kanuni na
taratibu zilizopo ili vyama hivyo viendelee kuwa imara zaidi katika utendaji
kazi.
Nyakunga amewakumbusha viongozi hao wa vyama vya Ushirika
kutokuwa sehemu ya migogoro kwenye vyama vyao hali ambayo hudhofisha vyama
hivyo katika kutekeleza majukumu yao kwa wanachama.
“tumeweza kuwasaidia ni namna gani wanaweza kusimamia vyama vyao
hata inapotokea migogoro juu ya vyama vyao kuweza kushugulikia migogoro hiyo na
kuitatua wao kama viongozi wa chama.
Restuta
Mussa mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo amesema wamejifunza mambo kadhaa
ikiwemo kupitishwa kwenye kanuni za kuujua vizuri ushirika na miongozo yake na
watakwenda kuya fanyia kazi yale waliyofundishwa.
“ugumu
wa kwanza ambao tulikuwa tunaupata hapo kabla ni elimu tulikuwa hatujapatiwa
elimu tunatalajia tukienda kule kwenye chama kitasimama kwa elimu hii” amesema
Restuta
Charles
Kapamba kutoka chama cha Msingi Ilunde amesema mafunzo hayo yanakwenda kuwa
chachu katika kuhakikisha chao kinafanya vizuri katika masuala ya ukaguzi kama
yalivyo fundishwa.
“kabla
ya mafunzo hayo tulikuwa na changamoto nyingi kunawakati inafika unampgia simu
afisa ushirika akuelekeze jammbo Fulani lakina kwa sasa hivi baada ya kupata
mafunzo haya naaamini mambo mengi kimsingi yatakenda vizuri”
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com