Baadhi ya Madiwani wa Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani [Picha na Walter Mguluchuma] |
Wiliamu Mbogo Diwani wa Kata ya Majengo akichangia hoja katika kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda[ Picha na Walter Mguluchuma] |
Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamelalamikia kitendo cha watoto wadogo kuzaa mitaani na kufanya biashara ya kuuza vyuma chakavu kwa wafanya biashara wa kununua vyuma chakavu .
Diwani
wa Kata ya Majengo Wiliamu Mbogo ameeleza kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la watoto
wadogo kuzagaa kwenye Kata ya Majengo na huku
wakiwa wamebeba vyuma chakavu .
Mbogo
ameshauri kuwa ni vema wafanya biashara wa vyuma chakavu wanao nunua kwa watoto
wadogo wakaonywa kuacha kufanya biashara
na watoto wadogo kwani wanasababisha watoto kuzurula na kueneo kwa wizi .
Amebainisha
kuwa hivi majuzi umefanyika wizi wa miundo mbinu ya vyuma vya
meza na viti vya chuma kwenye shule za Msingi za Azimo na Majengo ambavyo inasadikiwa vyuma hivyo
huuzwa kwa wafanya biashara wa vyuma chakavu ,
Diwani Mbogo ameeleza kuwa ni vema pia
wafanya biashara wa vyuma chakavu wakakumbushwa kutonunua chuma chochote kile cha Taasisi ya Seikali kwani kufanya hivyo ni kuihujumu Serikali
Diwani
wa Viti Maalumu Amina Kamande amesema kuwa tatizo la watoto kufanya biashara ya
vyuma chakavi ni kubwa .
Meya
wa Manispaa ya Mpanda Haidari Sumry amelieleza baraza hilo la Madiwani kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamira Yusuph
alisha waonya wafanya biashara wa vyuma chakavu kutofanya biashara hiyo
na watoto wadogo .
Ambapo
amesisitiza mfanya biashara atakae kutwa anafanya biashara hiyo na
watoto wadogo Dc Jamira alisema hatasita
kumfutia leseni yake ya biashara ameliambia baraza hilo la madiwani Meya Sumry