DC: BUSWELU AONYA UHARIBIFU WA MAZINGIRA


Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akigawa miti kwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya mlele wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika katika shule ya Msingi Utende[ PICHA na Paul Mathais]

Na Paul Mathias Mlele-Katavi

Jamii imeaswa kuendelea kutunza mazingira ikiwemo kupanda miti ikiwa nisehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi ambayo yanashuhudiwa kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini.

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akipanda mti katika shule ya Msingi Utende halmashauri ya Wilaya ya Mlele alipoongoza kampeni ya kupanda miti kwenye halmashauri hiyo.[PICHA na Paul Mathias]

Jamii imeaswa kuendelea kutunza mazingira ikiwemo kupanda miti ikiwa nisehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi ambayo yanashuhudiwa kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Onesmo Buswelu wakati akizindua kampeni ya upandaji wa miti iliyofanyika katika Shule ya Msingi Utende Buswelu, amesema  kuwa kwakutambua umuhimu wa Kuhifadhi mazingira kila mwanajamii anaowajibu wa kutunza Mazingira kwenye eneo analoishi.

Buswelu amebainisha kuwa serikali haitafumbia macho wale wote wenye tabia ya kuharibu mazingira kwa kukata miti hawatabaki salama kwani serikali ipo macho pamoja na taasisi za uhifadhi ikiwemo wakala wa mistu Tanzania Tfs pamoja na wadau wengine wa uhifadhi wa mazingira.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Telesia Irafay akisoma Taarifa ya utekelezaji wa Upandaji miti kwenye katika uzinduzi wa upandaji wa miti kwenye shule ya Msingi Utende[PICHA  na Paul Mathias]

Amesema miti hiyo iliyopadwa shuleni hapo ipatayo 2196 ilidwe na kutuzwa na kusiwepo na aina yeyote ya kuharibiwa na Mifugo kwakuwa kazi iliyofanyika nikwa masilahi ya uhai wa uhifadhi wa mazingira pamoja na viumbe hai kwakuwa uwepo wa miti mingi ndiyo chanzo cha mvua za kutosha ambazo hunyesha na kuufanya binadamu kufanya kazi kama kilimo na kazi zingine.

Aidha katikahatua nyingine ameagiza kuazishwa utaratibu wa uoteshaji wa Vitaru vya Miti katika maeneo ya shule na ofisi zingine katika ngazi ya Kata ili zoezi hilo liwe endelevu kwa wanachi kupanda miti pasipo kusubiria msukumo wa mamlaka za serikali.

Amesema kila kiongozi anapaswa kuwa balozi wa kuhifadhi mazingira kwakuwa swala la mazingira ni suala matambuka kwa kuwa linamhusu kila mmoja kwenye jamii yetu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Soudy Mbogo akipanda mti katika shule ya Msingi Utende ikiwa nisehemu ya kampeni ya upandaji miti katika mkoa wa Katavi.[PICHA na Paul Mathais]
Akisoma Taarifa ya utekelezaji wa Kampeni ya Upandaji wa miti kwenye halmashauri hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Telesia Irafay amesema halmasahuri ya wilaya ya mlele katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Dk Philipo Mpango juu ya upandaji wa miti kwaajili ya utunzaji wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji .

Amesema halmashauri hiyo imeanza kusambaza miti katika taasisi mbalimbali kwaajili ya kupanda miti hiyo kwenye maeneo hayo, Irafay amesema kuwa lengo lililopagwa na halamsahuri hiyo ni kupanda miti ipatayo milioni moja na lakitano na kuisimamia na kuhakikisha inafanyiwa uangalizi wa hali ya juu ili kuwa sehemu ya kutunza mazingira.

“kazi zilizofanyika ni kusafirisha miti hiyo kutoka eneo la uzalishaji na kuisambaza katika taasisi mbalimbali ndani ya halmashauri ya Wilaya ya Mlele lakini pia tumesimamia upandaji wamiti pamoja na kutoa maelekezo katika upandaji huo lakini tumetoa elimu juu ya umuhimu wa kupanda miti katika maeneo tofauti kama sehemu za baiashara na kaya” amesema Irafay

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Telesia Irafay Akipanda mti katika shule ya Msingi Utende ulipofanyika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti kwenye halmashauri hiyo.[PICHA na Paul Mathias]
Michael Msumeno mkazi wa Kijiji cha Utende ambae ameshiriki kupanda miti kwenye uzinduzi amsema “kuna umuhimu mkubwa wa kuapanda miti kwani husaidia kupata uoto wa asili kwaajili ya kupata mvua kwa sababu mvua inategemea miti na ninaimani serikali walichokifanya kinamaana sana nakiunga mkono”

Msumeno ametoa Rai kwa wanachi kutoendelea kuharibu mazingira kwa kukata miti kwani kufanya hivyo nikuhujumu Rasilimali za mazingira hali ambayo hupelekea ukosefu wa mvua.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Utende iliyopo halmashauri ya Wilaya ya Mlele wakiwa wamebeba Miti tayari kwaajili ya kuipanda kwenye shule yao ulipofanyika uzinduzi wa Kampeni ya upandaji miti kwenye halmashauri ya wilaya ya Mlele.
Nae Fabiana Katuma akiwa kwenye zoezi hilo la upandaji miti amebainisha kuwa kupanda miti ni kuhifadhi mazingira na kupata hewa nzuri ianayo tokana na miti pamoja na kupata maji kupitia miti na mambo mengine.

Kwa habari zaidi tembelea ukurasa Wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages