WAMACHINGA: KATAVI ASANTE RAIS SAMIA KWA KUTUONA

Wamachinga katika mkoa wa Katavi wakiwa kwenye zoezi la kukabidhiwa hati ya kiwanja kwaajili ya ujenzi wa ofisi yao eneo la kashaulili Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi[PICHA na Paul Mathias]
Na Paul Mathias-Katavi

Wafanya biashara wadogo wadogo maalufu kama wamachinga katika mkoa wa Katavi wameishukuru serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kulitambua Kundi hilo Rasimi kama makundi mengine.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko[kulia] akimkabidhi hati ya kiwanja Erinest Matondo Mwenyekiti wa shilikisho la umoja wa Machinga Taifa katika hafla ya makabidhiano  iliyofanyika viunga vya ofisi ya Mtendaji Kata ya Kashaulili Manispaa ya Mpanda[ PICHA na Paul Mathias].
Wafanya biashara wadogo wadogo maalufu kama wamachinga katika mkoa wa Katavi wameishukuru serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kulitambua Kundi hilo Rasimi kama makundi mengine.

Wamebainisha hayo wakati wa Makabidhiano ya Hati ya Kiwanja kilichotolewa na uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Katavi kama sehemu ya Maagizo ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kundi hilo kutambuliwa rasimi na kuwezeshwa miundombinu yao ili waweze kufanya kazi zao bila tatizo lolote.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Katavi Marko Ernest akitoa salamu za pongezi kwa serikali kwa kuwapatia Hati ya kiwannja kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya wamachinga mkoa wa katavi. 

Jennifer Evalist Mfanya biashara mdogo Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi amesema kupatiwa kiwanja na serikali ni hatua nzuri kwakuwa wao ni sehemu ya kuchangia pato kwa serikali kwa kazi wanazozifanya za baiashara ndogo ndogo.

“leo tumekabidhiwa Hati ya kiwanja kwaajili ya wamachinga kujenga ofisi yetu hii itatusaidia sisi Machinga kwaajili ya kuendeleza Shughuli zetu napenda kuishukuru Serikali kwa kutuwezesha wametuheshimisha tutajikwamua kiuchumi” amesema Jennifer

wamachinga Mkoa wa Katavi wakifurahia jambo wakiwa kwenye makabidhaino ya hati ya kiwanja kwaajili ya ujenzi wa wa ofisi yao.[PICHA na Paul Mathias].

Ameeleza kuwa imekuwa bahati kwa mkoa wa Katavi kwa kuwapatia eneo na kuahidi kufanya kazi kwa bidiii kwakuwa serikali inawatambua Rasimi sasa.

Nae Aliki Gabriel mmoja wa Machinga akizungumnza baada ya makabidhiano ya hati hayo kufanyika kwa wamachinga amesema anaushukuru uongozi wa mkoa kwa kuwapatia kiwanja kwa sasababu walikuwa wanapata changamoto ya kufanyia baishara zao.

“kwanza kabisa nipende kushukuruuongozi uliotupatia kiwanja kwa sasababu ilikuwa changamoto nyingi tulikuwa tunaziupata kabla hatujawa na sehemu ya kujenga ofisi leo hii tumeweza kupewa kiwanja kikubwa kuweza kujenga ofisi za wamachachinga nashukuru sana”

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ambae alikuwa Mgeni Rasimi katika makabidhiano hayo ya Hati ya kiwanja kwa wamachinga wa Mkoa wa Katavi amesema anaushukuru uongozi wa machinga taifa kwa kuwa na shirikisho litakalo saidia kutatua changamoto za wamachinga kwa kushirikiana na serikali.

“kutokana na umuhimu wenu wafanyabiashara ndogo ndogo mnafahamu kabisa kuwa na nimashuhuda kwamba Mh Rais Dk Samia suluhu Hassan tangu aliposhika madaraka amekuwa akifanya mambo mengi kuhusu nyie kuhakikisha kuwa mnatengenezewa mazingira mazuri,wezeshi na rafiki kwaajili ya kufanyia biashara zenu kwa ufanisi” amesema Mrindoko

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akiwahutubia wamachinga kwenye hafla ya kuwakabidhi hati ya kiwanja kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya wamachinga mkoa wa katavi.[PICHA na Paul Mathias]
Mrindokoameupongeza uongozi wa wamachinga Taifa kwa kuwa na shirikisho linalofanya kazi nchi nzima ambalo linawasaidia watendaji wa serikali kiutendaji katika kutatua changamoto za wamachinga.

Aidha katika hatua mkuu huyo wa mkoa amesema halmashari zilizopo katika mkoa wa Katavi ziendelee kutenga maeneo ya wamachinga pamoja na kuyawekea miundombinu rafiki sambamba na kuanzisha Madawati yatakayo ratibu maswala ya wamachinga kwenye ngazi ya halmashauri.

“na sisi kama mkoa tutasimamia kuhakikisha halmashauri zinaendelea kutenga maeneo kwaajili ya wafanya baisahara ndogondogo,pia halmashauri zote ziwe na Madawati maalumu kwaajili ya kuratibu na kuhudumia shughuli mbalimbali na mashauriano na wafanya biashara wadogo wadogo wamachinga” amebainisha mkuu huyo wa mkoa.

Mwenyekiti wa Shirikisho la umoja wa Machinga Mkoa wa Katavi  Marko Ernest amesema anamshukuru Rais Dk Samia suluhu hassan kwa kuagiza wamachinga kupatiwa maeneo kwaajili ya kujenga ofisi agizo hilo limetekelezwa katika mkoa wa Katavi.

Amesema hiki kilichofanyika kwao nitendo  mhimu sana kwa sababu watajenga ofisi ya kisasa na kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku kwakuwa watakuwa na ofisi ya kudunu.

Awali akitoa taarifa ya kazi za wamachinga katika mkoa wa Katavi Ana Shumbi amesema mkoa wa Katavi unajumla ya wamachjinga 3860 ambao wamekuwa wakiwatembelea kwenye maeneo yao juu ya utatuzi wa changamoto zao zinazo wakabili.

Ameatoa rai kwa wamachinga katika mkoa wa Katavi kuendelea kujiunga katika shirikisho ili serikali iwe na urahisi wa kuwasaidia pindi fursa mbalimbali zinazojitokeza serikalini kupitia kundi hilo

kwa habari zaidi endelea kutembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages