KIKOGWE ANYOFOLEWA MASIKIO NA MTOTO WAKE WA KUMZAA

 


Kituo cha Afya Karema alipolazwa winfrida Athanasi baada ya kunyofolewa masikio yake na Mtoto wake wa Kumzaa [Picha na Walter Mguluchuma]  

Mkazi wa  Kitongoji  cha  Kalilangwa Kijiji cha  Mchangani  Kata ya Ikola  Tarafa ya 
Karema Wilaya ya Tanganyika  Mkoa wa Katavi  Winfrida  Athanas(63) 
amenyofolewa masikio yake yote mawili  na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe baada ya kumvizia wakati akiwa amelala usingizi chumbani mwake .

Tukio hilo la kusikitisha  na la kikatili limetokea hapo juzi majira ya saa tano usiku chumbani kwa mama huyo alipokuwa amelala kitandani .

Afisa Mtendaji wa Kata ya Ikola Mwela Mrugwa amesema mama huyo amenyofolewa masiko yake mawili  na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe aitwaye  Michael Msapi (40).

Siku hiyo ya tukio  mtuhumiwa Michael Msapi alimvizia  mama yake mzazi wakati akiwa amelala  usingizi chumbani mwake  na ndipo alipoingia  ndani ya chumba hicho na kumnyofoa masikio yake yote mawili kwa kutumia meno yake na kumsababishia mama huyo maumivu makali sana .

Baada ya kuwa amefanya ukatili huu kwa mama yake mzazi mhumiwa huyo alitokomea baada ya kuwa mama yake amepiga mayowe ya kuomba msaada .

 Mwela  Mnugwa amesema baada ya majirani kusikia mayowe hayo walifika  haraka kwenye eneo hilo na kumchukua  Winfrida  na kumkimbiza haraka kwenye kituo cha Afya cha Karema ambako  hadi sasa anaendelea kupatiwa  matibabu .

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ally  Hamad  Makame  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limeripotiwa katika jeshi la Polisi. 

Amesema chanzo cha tukio hili ni  Imani za kishirikina  mtoto wa mama huyo  Michael Msapi kumtuhumu mama yake kumloga mtoto wake .

Msako mkali unaendelea wa kumsaka mtuhumiwa huyo kwani ametoroka mara tuu baada ya kufanya tukio hili  la kikatili.

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages