Na Paul Mathias- Mpanda.
Wazazi na walezi katika wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameonywa kutokuwa sehemu ya kuwakwamisha wanafunzi wa Darasa la awali, Darasa la Kwanza na Kidato cha kwanza kuanza masomo yao kwa mwaka huu wa 2023.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph wakati alipofanya ziara
ya kuangalia hali ya Kuripoti kwa wanafunzi katika shule ya Msingi Ilembo,Shule
ya Msingi Azimio,Shule ya Msingi Majengo na Shule ya Sekondary Mpanda Day
zilizopo halmashauri ya Mnispaa ya Mpanda.
Akiwa
katika Shule ya Sekondary Mpanda Day Mkuu huyo wa Wilaya amemshukuru Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha
kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa amabapo katika Manispaa ya Mpanda
wameafanikiwa kujenga vyumba 51 huku halmashauri ya Nsimbo wakifanikiwa kujenga
vyumba vya Madarasa 27 kwaajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka
huu 2023, Madarasa hayo yakiwa yameghalimu kiasi cha shilingi bilioni 1, na milioni 560.
Jamila amesema “tumegundua bado kuna wanafunzi mpaka sasa hivi bado hawajalipoti kuanza Darasa la awali,Darasa la kwanza na Kidato cha kwanza nitumie nafasi hii kutoa wito kwa wazazi na walezi wa wilaya ya Mpanda kuhakikisha mtoto yeyote aliefaulu kulipoti kwenye shule aliyopangiwa’’
Amebainisha
kuwa tayari wamesha waagiza viongozi kuanzia ngazi ya Mitaa,Vijiji, watendaji
na Mdiwani kuhakikisha wanahamasisha wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao
shule kwani hakuna kisingizio kingine kwasababu miundombinu ya Madarasa ipo
kwaajili ya wanafunzi hao.
‘’
mzazi yeyote ambae atazembea kutimiza huo wajibu wake wa kuhakikisha mtoto
anaenda Darasa la kwanza ama Darasa la awali na kidato cha kwanza hatutamuacha
tutamshughulikia kwa mujibu kanuni na taratibu za nchi hii amenena Jamila’’
Katika
hatua nyingine amesema wameluhusu watoto kulipoti shule na kuanza masomo hata kama
mzazi hajakamilisha taratibu za sale kwa mtoto wake hivyo hakuna kisingizio cha
mzazi kutompeleka mtoto shule.
Akisoma
taarifa ya hali ya uripoti kwa wanafunzi katika shule ya secondary Mpanda day
Mwalimu mkuu msaidizi Moliwe Sanga amesema mpaka sasa wavulana 98 wameripoti
shuleni hapo huku wasichana wakiwa 122 na kufanya jumla ya waliolipoti kufikia 200.
Sanga
ameeleza kuwa jumla ya wanafunzi 106 hawajaripoti Wavulana 44 na wasichana 62
na kufanya jumla ya wasiolipoti kufikia 106.Mwalimu mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondary Mpanda Day Moliwe Sanga akisoma taarifa ya kuripoti kwa wanafunzi kwa mkuu wa wilaya ya Mpanda jamila Yusuph [Picha na Paul mathias]
Awali
Akizungumnza mbele ya mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila yusuph ,Mwalimu Adelahida
Thomas Mwalimu wa Elimu maalumu katika shule ya Msingi Azimio ameiomba jamii
kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu kwani nao wanahaki ya kupata
elimu kama watoto wengine.
Akiwa katika shule ya Msingi azimo mkuu wa wilaya Jamila yusuph amepata fursa ya kuzungumnza na walimu pamoja na kutembelea miundombinu ya madarasa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu na kujionea ujenzi wa Bweni la wanafunzi hao ambalo limekamilika katika hatua ya kuezekwa.