SITA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MWALIMU NA KUMTUPIA NDANI YA MTO UGALLA .


Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Ali Makame Hamad akizungumnza na waandishi wa habari ofisini kwake wakati alipokuwa anatoa taarifa ya Matukio mbalimbali katika mkoa wa Katavi.
Na Walter Mguluchuma- Katavi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kumuua mwalimu wa Shule ya Msingi Ugalla Wilaya ya Mpanda na kisha kumtupia mtoni baada ya kumfumania akifanya mapenzi na mke wa mtuhumiwa mwenzao.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Ali  Hamad Makame amewataja watuhumiwa hao kuwa ni  Sud Athuman , Sangalo Said , Mrisho Hamis ,Juma Kanyama  Malim Anton na Taus Hamis wote wakazi wa Kijiji cha Ugalla Wilaya ya Mpanda .

Ameeleza kuwawatuhumiwa hao wote sita walikamatwa  mnamo Januari  9 mwaka huu majira ya saa nane usiku huko katika eneo la Kijiji cha Ugalla .

Kamanda Ali Makame  ameeleza  kuwa   mnamo tarehe  28 mwezi wa  12 mwaka jana  huko katika mto Ugalla  zilipokelewa taarifa  kuwa kuna mwili wa mtu  umeonekana  unaelea ndani ya maji ya  mto ugalla  ugalla ambae hakuweza kufahamika kwa jinawala surabaada ya kuwa mwili huo umeharibika vibaya .

Baada ya mwili huo kuwa umeopolewa ndani ya maji uchunguzi ulifanyika  wa kidaktari na ndipo ulipo unyesha kuwa mwili huu ulikuwa  na majeraha ya kupigwa na uliweza kutambuliwa kuwa ni mwili wa mwalimu wa Shule ya Msingi Ugalla   baada ya uchunguzi huo wa daktari  msako ulianza wa kuwabaini watu waliofanya mauaji hayo .

Kufatia msako huo mkali uliofanywa na Jeshi la polisi ndipo mnamo tarehe 9/1/2023 polisi walipo weza kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wote sita .

Kamanda Makame amebainisha kuwa  katika uchunguzi wa awali  umebaini kuwa  marehemu  kabla ya kuuawa  alifumaniwa  na mke  wa mtu  ndipo watuhumiwa hao waliamua kumpiga na kumtupia mtoni .

Watu humiwa wote  wanaendelea  kushikiliwa na Polisi na mara  baada ya upelelezi kuwa umekamilika  watafikishwa Mahakamani  kujibu tuhuma zinazo wakabili

    

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages