Welema Ochola Mkulima wa Pamba katika Kijiji
cha Mpembe amesema wanamatumaini makubwa baada ya kupatiwa Elimu na vifaa
kwaajili ya kupulizia Mashamba yao viwatilifu kutakuwa na ongezeko la
uzalishaji tofauti na msimu uliopita.
Ochola anasema”kabla ya kupata pembejeo hizi ambazo ni sumu kwa wadudu waharibifu,Pampu pamoja na viwatilifu vingine kweli tulikuwa tunapitia wakati mgumu sana pamba ilikuwa inashambuliwa na wadudu na kuharibika sana tunaishukuru Bodi ya Pamba na NGS mnunuzi wa zao hili kwa kutupatia elimu na vifaa hivi’’
Wakulima wa zao la Pamba katika kijiji cha Kapanga wakiwa kwenye hatua ya kupalilia Magugu Shambani walipotembelewa na watalamu wa Kilimo Kutoka Bodi ya Pamba mkoa wa Katavi.[Picha na Paul mathias] |
Kwa upande wake Mabula Lugendenga
Mkulima wa zao la pamba katika kijiji hicho amesema atakenda kuyafanyia kazi
maelekezo aliyopewa na wataalamu wa kilimo kwani anamatalajio ya uzalishaji
mkubwa kwenye ekali kumi alizolima msimu huu.
Mashauri Maduhu mkulima wa pamba katika jijiji
cha Kapanga amebainisha kuwa kunatofauti kati ya msimu huu na msimu uliopita
katika eneo la pembejeo kwa kuwafikia kwa muda hali ambayo inawafanya kwenda
sambamba na msimu wa zao hilo.
‘’mwaka huu naona kuna unafuu
kunamwitikio kwa watalamu kuja kutusaidia, nimelima ekali nane nashukuru NGS na
watalamu wa bodi ya pamba kwa elimu hii itaninufaisha kwenye kilimo changu
amesema Maduhu”
Ramadhani Dissa Mratibu wa kilimo
cha zao la Pamba kutoka Bodi ya Pamba mkoa wa Katavi ameeleza kuwa wamekuja
kusaidiana kuhakikisha msimu huu pamba yote iliyolimwa inafikia hatua ya
kuvunwa.
Dissa ‘’amesema Misimu iliyopita
walikuwa wanaotesha Pamba lakini inapofika wakati wa kutengeneza Vitumba inasahambuliwa
na wadudu na visumbufu vingine vya Pamba na tatizo kubwa lilikuwa kwenye
unyunyiziaji na vinyunyizi’’
Amebanisha kuwa Bodi ya Pamba
itahakikisha wakulima wote wanapata vinyunyizi na viwadudu vinavyotakiwa ili
kukidhi matakwa ya serikali.
Joseph Nyese mkaguzi wa Pamba
wilaya ya Tanganyika amesema bodi ya Pamba kwa kushilikiana ya na Kampuni ya NGS iliyopewa Ridhaa ya kusambaza pembe jeo
kwa wakulima wa zao la Pamba anasema wakuja na mpango maalumu wa kuzunguka
kutoa elimu ya matumizi sahihi ya viwatolifu na vinyunyizi.
Nyese amefafanua kuwa mpango huo
unakuja baada yakuona wakulima wengi kulalamika dawa kutofanya kazi waligundua
kuwa baadhi ya wakulima kutokuwa na elimu sahihi ya vinyunyizi hivyo ndio maana
wameanza kutoa mafunzo hayo kwa wakulima wakati huu wa kunyunyizia viwatilifu
kwewnye mashamba yao.