KATAVI : YATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA KWA VITENDO

 


Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiwa katika Bwawa la Milala Manispaa ya Mpanda alipotembelea na kujionea uhalisia wa Chanzo hicho cha Maji kwa Manispaa ya Mpanda ikiwa ni sehemu ya kuhakisha vyanzo vya Maji Vinalidwa.[Picha na Paul Mathias.]

Na Paul Mathias-Katavi 

Serikali katika mkoa wa Katavi imeanza kutekeleza Agizo la Rais Dk Samia Suluhu Hassan la kupanda miti ambapo miti  Milioni 4.7 katika kampeni ya Ng'alisha Katavi tunza mazingira katika kampeni maalumu iliyoanza Tarehe 24/1/2023 hadi 26/1/ 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua [Mrindo Mwenyekofia ]akishiriki kupanda Mti na Mwananchi katika Eneo la Mtaa wa Shanwe kilipo chanzo cha Maji cha Bwawa la Milala alipofika kwaajili ya kuzindua upandaji miti kimkoa.Picha na Paul Mathias

Serikali katika mkoa wa Katavi imeanza kutekeleza Agizo la Rais Dk Samia Suluhu Hassan la kupanda miti ambapo miti  Milioni 4.7 katika kampeni ya Ng'alisha Katavi tunza mazingira katika kampeni maalumu iliyoanza Tarehe 24/1/2023 hadi 26/10/ 2023

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Kampeni hiyo ya Upandaji mti Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alipotembelea Bwawa la Milala na Kupanda miti kwenye Bwawa hilo mkuu huyo wa Mkoa amesema

'tumeanza utekelezaji rasimi tarehe 24/1/2023 na utekelezaji ukaendelea Tarehe 25 na unaendelea leo 26/1/2023 ambapo tutakwenda kufikia kilele kwa awamu hii ya kwanza kwa mwaka 2023 lengo letu ni kupanda miti Milioni 10 mpaka sasa tumepanda miti zaidi ya milioni 4.7 kwenye halmsahauri zote kwenye taasisi za shule msingi na sekondari pamoja na kaya za mtu mmoja mmoja'' amesema Mrindoko.

Muonekano wa Bwala la Milala lililotembelewa na mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, Bwawa hilo linatajwa kuwa Mkoambozi kwa wananchi wa Manispaa ya Mpanda pindi utekelezaji wa mradi wa maji wa Miji 28 utakapotekelezwa.[PICHA na Paul Mathias]

Amewaasa wananchi wa mkoa wa katavi kuendelea kupanda miti katika maeneo yao ya makazi ikiwa nisehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kutunza Mazingira.

Mrindoko akiwa katika Bwawa la Milala amepiga marufuku kufanya Kazi yeyote ya kibinadamu kwenye chanzo hicho kwa kuwa ndicho chanzo kikuu Cha maji katika Mradi wa maji wa miji 28 ambao mkoa wa katavi nisehemu ya wanufaika na Mradi huo pindi utakapoanza kutekelezwa.

“Nitumie nafasi hii kupiga marufuku na kukataza kabisa shuguli za kibinadamu kuzunguka Bwawa la Milala kulima,Kuchunga Ngo”mbe,Kufuga,Kuvua Samaki,na kufanya shuguli nyingine ni marufuku nimesema bwawa hili ni bwawa mhimu nichanzo cha maji na ttutakilinda na kukitunza kwa kushirikiana na wanachi waliopo maeneo haya”

Katika hatua nyingine amewaomba wananchi walio karibu na Chanzo hicho  Bwawa  la Milala kuwa Mabalozi na walinzi wa vyanzo hivyo Kwa kutoa taarifa za Kwa mamlaka husika kama Kuna kiashria Cha uharibu wa mazingira na vyanzo vya maji kwenye bwawa Hilo zinazofanywa na binadamu.

Awali akitoa taarifa Kwa Mkuu wa mkoa wa Katavi Kaimu  Mkurugenzi wa Muwasa Manispaa ya Mpanda Justini Wambali amesema katika kulinda chanzo hicho Cha maji wamekuwa wakishirikiana Kwa pamoja  na wananchi kukilinda chanzo hicho kwa kutokufanya shughuli za kibinadamu.

Wambali ameeleza kuwa katika Mradi wa maji wa miji 28 utakwenda kuwa mkombozi wa utoaji wa huduma ya maji kwa wanachi wa Manispaa ya Mpanda kwani tayari mikataba baina ya serikali na wafadhili kutoka Serikali ya India  ulishasainiwa tayari kwa utekelezaji kwa Gharama ya shilingi Bilioni 22.

Katibu tawala Mkoa wa Katavi Hassan Abas Rugwa akiwakatika zoezi la upandaji miti katika moja yapo ya chanzo cha maji kwenye Bwawa la Milala[Picha na Paul mathias]
"Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Milala inkwenda kutatua kero ya upatikanaji ya hudua ya maji kkwa wananchi wa Manispaa ya Mpanda kwa asilimia miamoja kwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka Lita Milioni 6 na elfu 50 kwa siku hadi kufikia lita Milioni 19 na elfu 50 kwa siku ambapo mahitaji ya maji kwa kata 15 za Manispaa ya Mpanda ni lita Milioni 15".

Amesema Kwa Sasa bwawa Hilo linatumika kama chanzo cha Maji Kwa kutoa huduma ya maji katika baadhi ya maeneo ya kata ya shanwe na Eneo la chuo Cha Veta Mpanda.

Hamisi Mrisho mkazi wa Bwawani amesema aungamkono agizo la mkuu wa Mkoa la kupiga marufuku kazi za kibinadamu kwenye Bwawa la Milala  na kuhakikisha wao kama wakazi wa eneo jirani na chanzo hicho cha bwawa watakuwa sehemu ya kulinda na Kutunza vyanzo vya Maji kwa vitendo.

‘’Kwa kuwa zoezi hili la upandaji miti ni endelevu naunga mkono agizo la Mkuu wa mkoa” amesema Mrisho.

Kwa upande wake Anjelina Lucas mkazi wa kivukoni  akiwa katika chanzo hicho Cha maji Cha bwawa la Milala amesema Kila mwanananchi anawajibu wa kutunza Mazingira Ili kulinda vyanzo vya maji.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwana Mvua Mrindoko[Kushoto ]akimkabidhi Mti kwaajili ya kuupanda Mkurugenzi wa Jukwaa la Vijana Mkoa wa Katavi Saimon Jonh katika uzinduzi wa Kampeni ya upandaji miti ambapo mkurugenzi huyoalikuwa sehemu ya kushiriki katika zoezi hilo[PICHA na Paul Mthias]

‘’tumeambiwa kwamba tutunze mazingira moja ya kutunza mazingira ni pamoja na kutokata miti kulima pembezoni mwa bwawa hili na mengine mengi yaliyozungumzwa ambayo yanachangia uhalibifu wa Bwawa letu hililinalotuletea vyanzo vya maji"

amesema miti iliyopandwa katika eneo hilo wataitunza na kuisimamaia iweze kukua na kuwa sehemu ya kutunza vyanzo vya maji katika eneo hilo.

"tumeshiriki kupanda miti kwenye Bwawa hili  na sisi kama wananchi tupo Pamoja na Serikali kutunza rasilimali maji Kwa kutunza Mazingira na kupanda miti’’ .

Kampeni ya kupanda miti katika mkoa wa katavi inayojulikana kama Ng'alisha katavi tunza Mazingira inalengo mahususi ya kulinda mazingira na vyanzo vya maji kama sehemu ya tekelezo agizo la Serikali la kupanda miti kama sehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages