Mjumbe wa Halmshauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM kutoka Mkoa wa Katavi akiwahutubia wanawake wa Jumuiya hiyo ya UWT Mkoa wa Katavi[Picha na Alex Ngereza] |
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Gilbert Sampa amewataka Umoja wa jumuiya ya wanake ya chama cha Mapinduzi UWT Mkoa wa Katavi kutumia fursa ya kuwekeza miradi ambayo itakuwa na tija kwenye umoja wao.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Gilbert Sampa amewataka Umoja wa jumuiya ya wanake ya chama cha Mapinduzi UWT Mkoa wa Katavi kutumia fursa ya kuwekeza miradi ambayo itakuwa na tija kwenye umoja wao.‘’Nyie kama UWT mnao uwezo wa kuanzisha vitega uchumi vitakavyo wasaidia kuiendesha jumuiya kwa kujikwamua kiuchumi kama chama chetu kinavyo sisitiza kubuni Miradi kwenye Jumuiya za chama chetu”amesema sampa.
Katibu wa itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda Elias Mwanisawa akitoa neno kwa wanawake wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Katavi.[PICHA na Alex Ngereza] |
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi Fotunata Kabeja ameshiriki katika zoezi la upandaji miti katika ofisi za chama hicho wilaya ya Mpanda pamoja na kuwatembelea wagojwa katika kituo cha afya Town Clinic.
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda Elias Mwanisawa akitoa neno katika hafla hiyo amesema kila mwanachama anawajibu wa kuyatangaza kwa kifua mbele yale yote yaliyotekelezwa na Serikali ya Dk Samia Suluhu Hassan kwa vitendo.
“ndugu viongozi tusikubari mtu atakayeonekana kubeza juhudi ambazo Rais wetu amezifanya kwa nguvu kubwa”amesema mwenezi huyo.kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com