Wananchi katika halmashauri ya wilaya ya mlele mkoa wa Katavi wametakiwa kutofanya kazi za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji ili kuendelea kuhifadhi vyanzo hivyo.
Wananchi katika halmashauri ya wilaya ya mlele mkoa wa Katavi wametakiwa kutofanya kazi za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji ili kuendelea kuhifadhi vyanzo hizo.Mhandisi Girbert Aizaki Meneja wa Ruwasa Mlele akipanda Mti kwenye chanzo cha maji kinacho patikana katika Bwawa la Nsekwa haklmashauri ya Wilaya ya Mlele[Picha na Paul Mathias]
Akizungunza mara baada ya kuhitimisha zoezi la upandajimiti katika vyanzo vya Maji kwenye bwawa la Nsekwa lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amesema serikali imewekaza fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 2.8 kwaajili ya ujenzi wa mradi huo hivyo vyanzo vyake lazima vitunzwe.
“kwanini tumechagua kuja kupanda miti kwenye
eneo hili mnaloliona ni bwawa ambalo Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameleta
Bilioni 2.8 za kujenga bwawa hili ili tukusanye Maji ya kutosha kwaajili ya
wakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele wapatao Sabini na tano elfu”
Buswelu amebainisha wale waote waliovamia na
kuanza kufanya shuguli zakilimo karibu na kingo na mikondo ya kutililishia maji
kuelekea kwenye bwawa hilo waondolewe kwa mazungumnzo ya kuwaelimisha juu ya
umuhimu wa vyanzo vya maji na Bwawa hilo kwa ujumlaMkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akipanda mti kwenye moja ya chanzo cha Maji katika Bwa la Nsekwa halmashauri ya Wilaya Mlele[PICHA na Paul Mathias]
“Hawa wanaoonekana kufanya kazi kilimo kwenye
baadhi ya maeneo ya vyanzo vya maji vinavyotililisha maji kwenye bwawa hili
waiteni na muwaelimisha juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na muwaeleze
umuhimu wa bwawa hili yawezekana hawajawahi kufika na kuliona bwawa hili”amesetitza
Buswelu
Amesema mkoa wa Katavi chini ya mkuu wa mkoa wa
Katavi Mwanamvua Mrindoko wamekuja na
mpango huo wa upandaji miti mkoa mzima ili kuhakikisha Mazingira yanatunzwa ikiwemo
vyanzo vya Maji kwa masilahi ya vizazi vya sasa navya Baadaee.
Katika kampeni hiyo ya Upandaji Miti
iliyofanyika kwa muda wa siku mbili kwenye halmashauri ya wilaya ya mlele Jumla
ya miti ipatayo 8896 katika maeneo mbalimbali ikiwemo Shuleni,baadhi ya Maeneo
ya Mji wa Inyonga pamoja na maeneo ya vyanzo vya maji vinavyozukunguka Bwawa la
Nsekwa.Baadhi ya Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Mlele wakiwa wamejumuika na wanachi kwenye upandaji miti kwenye vyanzo vya Maji vinavyozunguka Bwawa la Nsekwa.[Picha na Paul Mathias]
Kwa upande wake Meneja wa mamlaka ya Usambaji
wa maji Vijijini Ruwasa Wilaya ya Mlele Mhandisi Girbert Aizaki amesema wao
kama Taasisi ya usambazaji maji vojijini kwa kushirikaina na wadau wengine wa
mazingira kwa pamoja wamekuwa na mipango shrikishi kwa kuhakikisha vyanzo vya
amaji vinalidwa muda wote.kwa kuwahusisha vijiji vinavyozunguka bwawa hilo.
“tunatoa wito sana kwa wanachi wa vijiji vya
Nsekwa,Mtakuja,Wachawaseme,na Kanoge,ili waweze kuwa familia katika utunzaji na
uhifadhi wa Bwawa hili kwa sababu,wanapoendelea kulima karibu na Bwawa maana
yake watasabisha mmomonyoko wa udongo nakusabisha tope nyigi kujaa kwenye Bwawa
hatuta kuwa na tena na bwawana pes azote ziliwekezwa na serikali zitakuwa
zimeharibika bure”ameonya Mhandisi Girbart.Wananchi mablimbali na wadau wa mazingira wakiwa katika zoezi la upandaji miti wakipanda miti kwenye chanzo cha Maji kwenye Bwawa la Nsekwa.[PICHA na Paul Mathias]
Wananchi walioshiriki katika zoezi la kupanda
miti kwenye vyanzo vya maji wamesema kuwa hatua hiyo itakwenda kusaidia kulinda
hifadhi ya kingo za mito zinazo mwaga maji kwenye Bwawa hilo hali ambayo itakayopelekea
upatikanaji wa maji ya kutosha.
Kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com