Moja ya shamba la Tumbaku mkoa wa Katavi ambapo wakulima wamelalamikia kukosekana kwa Mbolea aina ya CAN[ PICHA na Walter Mguluchuma] |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Wakulima wa Tumbaku Mkoani Katavi wamelalamika kukosekana kwa mbolea ya kukuzia aina ya CAN wakihofia kupata hasara wameiomba Serikali irudishe utararibu wa zamani wa Makampuni yanayonunua tumbaku yaruhusiwe kusambaza mbolea yenyewe.
Muonekano wa shamaba la Tumbaku katika katika kijiji cha Mchaka mchaka wilaya ya Tanganyika likiwa limekosa mbolea aina ya CAN kwaajili ya kukuzia [Picha na Walter Mguluchuma]
Wakulima wa Tumbaku Mkoani Katavi wamelalamika kukosekana kwa mbolea ya kukuzia aina ya Can wakihofia kupata hasara wameiomba Serikali irudishe utararibu wa zamani wa Makampuni yanayonunua tumbaku yaruhusiwe kusambaza mbolea yenyewe.
Wakizungumza na mwandishi wa Habari hii kwa nyakato tofauti wakulima hao wamedai kuwa huenda msimu huu wakapata hasara kubwa kutokana na kuvuna tumbaku isiyo na ubora .
Wamedai
kuwa mbolea ya can huchanganywa na mbolea ya NPK kwa ajiri ya
kukuzia tumbaku lakini pamoja na muda wa kumadia mbolea hiyo
kuwa imefika muda mrefu sasa lakini bado hawaja ipata .
Mwenyekiti wa Amcos ya Utense Helmani Katala amesema toka walipo panda tumbaku yao mwezi Novemba mwaka jana hadi sasa bado hawaja ipata .
Ameeleza kitaalamu mkulima hutakiwa kusamadia mbolea ndani ya siku saba hadi 14 baada ya kupanda lakini ni Zaidi ya miezi miwili sasa mkulima haja samadia jambo ambalo ni hatari kubwa kwa mkulima kuweza kukosa mapato .
Mkulima wa
AMCOS Mpanda Kati Nassor Ramadhan ameiomba
Serikali iangalie utaratibu uliokuwepo awali wa
Kampuni za ununuzi wa Tumbaku kusambaza mbolea kwa wakulima .
Amebainisha
siku hizi wanapata mbolea kupitia chama kikuu cha ushirika
LATCU tumbaku inakaribia kuvunwa kwa hiyo hata leo mbolea hiyo
ikiletwa haina faida kwa baadhi ya wakulima amesema Ramadhan.
Kokosekana
kwa mbolea hiyo kunawafanya wao kuzalisha tumbaku ambayo itakuwa
haina uzito unao takiwa na kusababisha uzalishaji wao kuwa mdogo na
tumbaku isiyo na ubora .
Ameeleza
wakulima wa tumbaku wamekuwa wakihimizwa na kusisitizwa kulima na
kupanda kwa wakati na sasa wamefanya hivyo hata hivyo wapo hatarini
kula hasara .
Kauli hii
imeungwa mkono na Richald Kasogera wa Amcos ya
Ilela Wilayani Mlele akisema kuchelewa kwa mbolea
kunasababisha ubora wa tumbaku .
Pia uzito nao
hupungua na kufanya mkulima zalisha chini ya
malengo yake na kusababisha hasara kwa mkulima .
Nae Deus
Bathromeo wa Igagala Wilaya ya Tanganyika amesema
tumbaku ikikuzwa na Npk peke yake huwa na rangi ambayo sio ya
chunjwa inayotakiwa kuwa nayo .
Hali hii
ni tofauti kwa wakulima wa Amcos ya Majalila
amesema wao hawana tatizo hili .
Mwenyekiti
wa chama kikuu cha ushirika LATCU Mkoa wa Katavi Venance
Dorashazi amemwambia mwandishi wa habari hizi kuwa wanatarajia
kuipata mbolea ya can wakati wowote wiki hii.
Amesema
wamewasiliana na muungano wao wa vyama vikuu vya ushirika vya mikoa ambao
wanao wamewasiliana na YARA kwa hali hiyo tatizo hilo litatatuliwa
shida ilikuwa ni kutofika mbolea hii kwa mapema .
Amesema
Amcos za Mishamo kuwa ndio zimeathilika Zaidi kwa kuwa hata cani
ikifika haitakuwa na kazi yoyote kwa kuwa wameisha anza kuvuna tumbaku na
kuvichoma .
Pia ameeleza kuwa hata kwenye Amcos za Mpanda Kati , Nsimbo Ilele , Utense na Ilunde endapo kama wiki hii itapita bila kuwa wamepata mbolea haita ikifika baada ya hapo haitakuwa na kazi tena .
Kwa habari zaidi Tembelea ukurasa wetu wakataviclub.blogspot.com