MEYA :SUMRY ANG'AKA POSHO WENYEVITI WA MITAA

 

Msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry wakati akifunga kikao cha Baraza la madiwani [Picha na Walter Mgluchuma]

Na Walter Mguluchuma –Mpanda

Meya  wa Manispaa ya Mpanda Haidari Sumry ameagiza kuanzia sasa Wenyeviti wote wa Mitaa kwenye Halmashauri hiyo kulipwa posho zao kwa wakati. 

Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani [Picha na Walter Mguluchuma]

Sumry ametowa amaagizo hayo  wakati  alipokuwa akifunga kikao cha Baraza la Madiwani  kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda .

Amesema kuwa licha ya wenyeviti wa Mitaa kufanya kazi kubwa sana lakini wamekuwa wakicheleweshewa kulipwa posho zao .

Amebaisha kuwa  Wenyeviti hao wamekuwa wakifanya kazi saa  24 za kusimamia Amani na kusuluhisha  migogoro mbambali kwenye maeneo yao .

Hivyo kama Manispaa  ni vema wakatambua mchango wa kazi wanazo fanya  kwa kuwatia moyo kwa kuwalipa posho zao kwa wakati kwani ni haki yao ya msingi .

Aidha Sumry amewaomba wandishi wa Habari waendelee kuwa hamasisha wananchi ambao watoto wao hawajaripoti shule waweze kulipoti .

"Kwani kuanzia Tarehe moja februari msako mkali utafanyika kwa wazazi wote ambao hawtoto wao hawajaripoti shule hivyo wasiilaumu Serikali pindi"amesema Haidary .

kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages