MBUNGE AWAFARIJI WAGONJWA SIKU YA MWAKA MPYA HOSPITALI YA RUFAA KATAVI.

 

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini,Sebastian Kapufi (kulia) akiwasalimia wangojwa walio katika hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Katavi alipowatembelea siku ya mwaka mpya 2023.

Walter Mguluchuma na Paul Mathias,Mpanda.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini ameungana na wagojwa katika hospital ya Rufaa Mkoa wa Katavi kwa kuwatembelea na kutoa zawadi ya Mwaka mpya kama ishara ya upendo na faraja kwao na kuwafikishia salamu za Rais Dk Samia suluhu Hassan za upendo ili waweze kupona haraka.

Baadhi ya wangonjwa akisalimia na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini,Sebastian Kapufi alipowatembelea.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini ameungana na wagojwa katika hospital ya Rufaa Mkoa wa Katavi kwa kuwatembelea na kutoa zawadi ya Mwaka mpya kama ishara ya upendo na faraja kwao na kuwafikishia salamu za Rais Dk Samia suluhu Hassan za upendo ili waweze kupona haraka.

Amesema pamoja na salamu hizo ameona aje kuungana na wagojwa hao katika kuukalibisha mwaka  .

Ameeleza zawadi anazowapatia ni ishara ya upendo wake kwao ikiwemo Sabuni,Juice ili ziwasaidie katika kujikimu wakiwa hospitalini hapo.

Kapufi mebainisha kuwa Rais Dk Samia Suluhu Hassani anawaombea afya njema ili Mlejee katika majukumu yenu ya Ujenzi wa Taifa.

Mwajuma Mbanga Muuguzi mfawidhi Hospitali ya Rufaa mkoa wa katavi amesema wanamshukuru Mbunge Kapufi kwakuona nivyema kabisa kuja kuwasalimia wagojwa lakini pia kuwatakia faraja na kuawapa chochote kitu kwa hali zao.

Amebainisha kuwa wanaendelea kumkaribisha kufika hospitalini hapo kwaajili ya kuwashika mkono wagojwa na kuwapatia ulichonacho.

Irene amos mmoja wa wagojwa walio juliwa hali na Mbunge huyo amesema Mungu ambariki kwa moyo wake wa upendo aliouonyesha kwa wagojwa hospitalini hapo.

Nae Anastazia Jonas anaemuuguza motto wake ameshukuru Mbunge wake Kapufi kwa zawadi alizowapatia

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages