MBUNGE KAPUFI AOBWA KUSAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO YA HOSPITAL YA MKOA

 

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi akiwa kwenye ofisi ya Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa Mkoa wa katavi alipotembelea ofisini kwake.

Na Walter Mguluchuma,Katavi

Mganga  Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi   Dkt Serafini  Patrice amemwomba Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini aweze  kwenda kuwasemia Serikali   juu ya changamoto inayoikabili Hospitali hiyo ya kutokuwa na gari hata moja la Hospital.

Mganga Mafawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi Dkt Serafini Patrice akitoa maelezo machache ya huduma hospitalini hapo alipotembelewa na Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani kapufi ofisini kwake.

Mganga  Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi   Dkt Serafini  Patrice amemwomba Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini aweze  kwenda kuwasemia Serikali   juu ya changamoto inayoikabili Hospitali hiyo ya kutokuwa na gari hata moja la Hospital.

Ameomba pia  akawasemee na kuhusu shida  walionayo  na  MSD  ambao wanavitu vingi sana vya kuleta katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi lakini  lakini wanavichelewesha .

Ombi hilo amelitowa wakati  wakati  alipokuwa akizungumza na Mbunge huyo ofisini kwake mara baada ya kuwa amemaliza  kuwafariji wagonjwa walilazwa katika Hospitali na wale walikuwa wakitibiwa ambapo aliwafariji kwa kuwapatia vitu mbalimbali vikiwepo pampasi za watoto na watu wazima   sabuni na Juice.

Amesema  Hospitali hiyo haina gari hata moja la ofisi wanatumia gari zao binafsi  ndogo kwani Hospitali hiyo haijawahi kuwa na gar la ofisi  waliazimwa na gari moja na Wizara ambalo nalo ni mbovu  ambalo limeharibikia Dodoma.

 Dkt  Patrice amefafanua kuwa gari hilo  ambalo waliazimwa na Wizara  limeharibika huko huko Dodoma wakati  lilipokuwa ilimepelekwa kufanyiwa  matengenezo huko   Dodoma .

 Amesema wanashida na  Bohari Kuu ya dawa (MSD) hivyo wanamuomba Mbunge Kapufi  aende akawasemee kwani wanavitu vingi  vya kuleta huku lakini wanachelewesha .

 Amebainisha  kuwa vifaa vya thamani ya nusu ya bilioni  5.9 ambavyo havija fika kwa ajiri ya Hospitali Mpya lakini havija fika bado na vilitakiwa view vimefika toka mwezi Desemba mwaka jana .

 Mganga huyo amesema kuwa timu yake wamejipanga kutowa huduma  za kipekee na bora kwa wateja wake  na ameishukuru Serikali kwa kuwaletea madakta nane wapya kwani waliokuwepo walikuwa saba .

 Mbunge Kapufi  amesema Serikali imekuwa sikivu kwa kuendelea kutatua changamoto kwa kuendelea kuleta wataalamu wa afya kwenye Hospitali  kadri inavyowezekana ili kuepusha mtumishi mmoja kihudumia watu wengi .

Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastiani kapufi akitembelea Wodi ya wagojwa na kuwapa pole siku ya Mwaka mpya 2023
Kwanza anaendelea kuishukuru Serika ya Rais Dkt Samia  Suluhu Hassan  kwa kadri anavyo sogeza huduma karibu na wananchi   wakati mwingine shida inakuwepo  kutokuwepo na vifaa tiba endapo  kama Msd  wataendelea na ucheleweshaji wa vifaa tiba .

Kunapo kuwepo  na  vifaa tiba hata kazi ya Daktari inakuwa rahisi  hivyo watumishi wa afya wasichoke kufanya kazi pindi inapokuwa kuna uchache wa vifaa.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages