Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi akiwa katika ziara ya kukagua Miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mfuko wa Jimbo |
Watalamu wa katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wameaswa kuzisimamia fedha za mfuko wa Jimbo kwa uadilifu ili zilete matokeo makubwa kwa wananchi kupitia Miradi ya maendeleo.
Wajumbe wa kamati ya mfuko wa jimbo la Mpanda Mjini wakiwa na Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo |
Watalamu wa katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wameaswa kuzisimamia fedha za mfuko wa Jimbo kwa uadilifu ili zilete matokeo makubwa kwa wananchi kupitia Miradi ya maendeleo
Rai
hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi wakati akiwa
katika ziara ya kutembelea na Kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mfuko wa
Jimbo 2021/2022 ili kulahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Kapufia
amesema kuwa kazi kubwa ya mfuko wa Jimbo ni Kuchochea na kusukuma maendeleo ya
miradi mbalimbali kwa wananchi hivyo watalaamu wanaowajibu wa kufatilia na
kufahamu mienendo ya Fedha hizo kwenye miradi katika maeneo yao kwa kina amesema
kapufi
Ameeleza
kuwa amelidhiswa na miradi hiyo licha ya baadhi ya miradi kuonekana kusuasua
licha ya fedha hizo kutolewa na kuwaomba watendaji wa serikali kuzitumia fedha
hizo kwa malengo yaliyokusudiwa kulingana na uhitaji wa maeneo husika
Katika
hatua nyingine ameeleza kulidhishwa na majitolea ya wananchi katika miradi hiyo
kwakuwa inaleta muunganiko mzuri kiutendaji baina yao na serikali hivyo miradi
hiyo pindi inapokamilika kuwa sehemu ya umiliki wa wanachi wenyewe.
Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini akiingia katika moja ya mradi unaotekelezwa na Mfuko wa jimbo wakati wa kutembelea na kukagua miradi hiyo. |
Kadala
amewaomba wafanyabiashara hao kuitunza Miundombinu hiyo ili iwezekudumu kwa
muda Mrefu kwa munufaa ya sasa na baadae.
Kwa
upande wake Maria Jonh mfanyabiashara wa Samaki katika siko la Kawalyowa
amemshukuru Mbunge huyo kwa kuahidi kupaua eneo la soko hilo kwa Shilingi
Milioni 10 ili waweze kufanya baishara zao katika mazingira Mazuri ya kiangazi
na masika.
Katika ziara hiyo Kamati ya Mfuko wa jimbo ikiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi wameweza kutetembelea miradi Kumi kati ya kuminamoja inayochochewa na Mfuko huo wa jimbo yenye Samani ya Shilingi Milioni 41,000,000