RC MRINDOKO ACHAFUKWA FEDHA ZA LISHE KUTOTENGWA


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua, Mrindoko akizungumnza katika kikao cha kujadili tathimini ya hali ya Lishe mkoa wa katavi kilichoshirikisha wadau wa sekta ya afya na wataalamu wa Afya [Picha na Paul Mathias] 

Na Paul mathias -Katavi

Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko ametoa siku Saba Kwa Wakurugenzi watendaji wa halmashauri,Maafisa lishe,na Waganga wakuu kumpatia taarifa za maandishi kwa kushidwa kutekeleza mikataba ya lishe kama inavyoelekeza.

Wajumbe mbambali wakiwa katika kikao cha kupitia tahimini ya lishe na masuala mbalimbali yanayo husu afya ikiwemo uzazi salama kwa wanawake na huduma za mama na mtoto[Picha na Paul mathias]
Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko, ametoa siku Saba Kwa Wakurugenzi watendaji wa halmashauri,Maafisa lishe,na Waganga wakuu kwenye halmashauri hizo  kumpatia taarifa za maandishi kwa kushidwa kutekeleza mikataba ya lishe kama inavyoelekeza.

Agizo Hilo amelitoa katika kikao cha kujadili Tathimini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe,Mkakati wa kuzuia Magojwaya Mlipuko na Utoaji wa huduma za Afya ya Mama na Mtoto Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Mpanda social hall Mpanda Mjini.

“Suala la utoaji wa Fedha za Lishe kwenye halmashauri zote halijafanyika vizuri kwa maana kipindi hiki  ilitakiwa iwe kwa Asilimia miamoja kwa fedha zote zinazo husiana na kipindi cha Miezi 6 kuhusu Lishe lakini hapa kuna Manispaa ya Mpanda ina asilimia 73 hawa wengine chini ya ishirini chini ya Hamsini hawa kutoa kabisa”amesma Mrindoko

amesema kwa mara kadha kumekuwapo na vikao vya kupeana maelekezo kuhusu utoaji wa Feha za lishe kwenye halmashauri hizo lakini utekelezaji wake umekuwa unakwenda kwa mwendo wa kinyonga.

Wajumbe mbambali wakiwa katika kikao cha kupitia tahimini ya lishe na masuala mbalimbali yanayo husu afya ikiwemo uzazi salama kwa wanawake na huduma za mama na mtoto[Picha na Paul mathias]
“hatuta mvumilia mtu yeyote Mtumishi yeyote ambae atakawamisha Mkataba wa lishe na hapa naona kunavigezo mhimu sana tusipochukua hatua Madhubuti mwaka huu tutajikuta tuna shidwa kuutekeleza Mkataba huu” amessisitiza

Hatua hiyo ikamlazimu mkuu wa mkoa kutoa maelekezo kwa Wakurugenzi watendaji,Waganga wakuu na Maafisa lishe kuwajibika kwa maandishi kufuatia hatua hiyo ya kushidwa kuutekeleza mkataba huo wa lishe kwenye Halmashauri zao

“Nikutake katibu tawala wa mkoa nataka nipate maelezo ya Wakurugenzi kwa maandishi kwanini wameshidwa kutekeleza utengaji wa fedha za afua ya Lishe,kwa mamalaka uliyonayo katibu tawala ya kiutumishi kwanini Ma DMO tusiwachukuliea hatua,kwanini tusiwachukulie hatua za kinidhamu Maafisa lishe , wote kwa mamlaka uliyopewa katibu tawala watoe maelezo ya maandishi kila mtu kwa jina lake kwa kushidwa kutekeleza agizo la Mh Rais la kutenga bajeti ya Feha za lishe na maelezo hayo niyapate ndani ya siku saba” amesema Mrindoko

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko [wanne kulia]akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya watalamu wa afya,wenyeviti wa halmashauri,kamati ya ulinzi na usalama mkoa na wadau mbalimbali wa Sekta ya afya katika mkoa wa Katavi[Picha na Paul Mathias]

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amekataa kupokea taarifa ya hali ya Afua ya lishe ya Mkoa kutokana uwasilishwaji wake kutokuwa katika hali ya Msawazo kwa kisingizio cha Mfumo kutofanya kazi hali iliyopelekea baadhi ya taarifa mhimu kukosekana kwenye uwasilishwaji huo.

Mrindoko ameendelea kuhamasisha wadau mbalimbali Kwa kushirikiana na Serikali kuendelea kupambana na Hali ya udumavu iliyopo ya asilimia 33.7 na ukondefu Kwa asilimia 3.9 Kwa kuwa Mkoa wa katavi unavyakula vingi samaki.

''Samaki tunao,viazi tunavyo na tuna Kila kitu kinachoitwa chakula katika mkoa wetu hivyo Kila Mmoja wetu anawajibu wa kuhakikisha watoto wanapata lishe Bora''

Ametoa maelekezo kuhakikisha Elimu ya masuala ya lishe Bora ianze kutolewa katika ngazi ya vitongoji kwa kutoa Elimu kupitia njia mbalimbali Ili kuwa na mkoa wenye watu wenye uwezo wa kufikili vizuri na kuepuka Udumavu.

Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi Iddy Hassan kimanta amesema Hali hiyo ya taarifa za watalamu kutolewa Kwa mfumo usiokuwa wakulidhisha umekuwa unajirudialudia hii haikubaliki.

‘’Niliwahi kuonya kwenye Kikao changu Cha kwanza Cha RCC taarifa za watalamu zinaanza kugawiwa siku ya kikao mkitaka sisi chama tuwaseme tutasema kwenye chama’’

Wajumbe wa kikao cha kutathimini hali ya huduma ya afya pamoja na masuala ya lishe Mkoa wa katavi wakiwa katika kikao hicho Mapema leo[Picha na Paul mathias]

Kuhusu Suala la Lishe Kimanta amesema lishe ni Suala mtambuka na kuwaasa watendaji kuliona Suala Hilo kuwa lenye umuhimu Mkubwa kwakuwa lishe ndiyo inayoandaa wafunzi katika kufikili wawapo masomoni na katika maisha yao Kwa ujumla

''Mimi ni Mzaliwa wa katavi napoona mambo kama haya watalamu hamututendei Haki mnamtaka nini Mkuu wetu wa mkoa wa mkoa ,kwenye hili la Lishe sijalizika nalo''amesema kimanta.

Katika kikao hicho wanchi wamekubushwa kuzingatia kanuni Bora za afya ikiwemo kuwa na Vyoo Bora Ili kuepuka magojwa ya mlipuko pamoja na kuzingatia kanuni Bora za afya ilikuwa na afya iliyonjema.

Kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages