Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametoa siku saba kwa Mkandarasi Suma JKT anaetekeleza Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa katavi kuhakisha anasambaza umeme kwenye jengo la Hospital iliyopo eneo la kazima Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Agizo hilo amelitoa wakati akipokea vifaa vitakavyopotumika kusambaza umeme kwenye jingo hilo alipotembelea hospitali hapo ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Waziri mkuu Kassimu Majaliwa alipofanya Ziara ya Kikazi katika mkoa wa Katavi mwaka jana na kuagiza umeme kusambazawa kwenye Jengo hilo la hospitali.
Amesema “lakini
nimwagize Mkandarasi Suma JKT tumempa siku Saba kuhakikisha kazi hii ya
kuingiza umeme huu ndani inakamilikai na ifikakapo Tarehe 15/1/2023 hii kazi
iwe imekamilika na huduma hapa zitolewe”
Amemwelekeza
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi Serafini Patrce kuhakisha kuwa vifaa tiba vyote vilivyoletwa na
serikali kukaka sehemu husika tayari kwa kuanza kufanya kazi ya kuhudumia
wananchi baada ya kumalizika kwa kazi ya kusambaza umeme katika jenngo hilo la
Hospitali ya Rufaa Mkoa wa katavi.
Aidha katika hatua amewaomba wanachi wa mkoa wa katavi kujisikia fahari kwa serikali yao ya awamu ya Sita ya Dk Samia Suluhu Hassani kwa uwekezaji katika sekta ya afya hasa kwa ujenzi wa hospitali ya rufaa mkoa wa katavi ili wananchi wapate huduma mbalimbali bila kufuata huduma hizo mikoa mingine.
Ni moja ya majengo yanayopatikana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambapo imeigharimu serikali kiasi cha fedha zaidi ya Bilioni 12 kwenye ujenzi wake. (Picha Na George Mwigulu) |
Ni moja ya majengo yanayopatikana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambapo imeigharimu serikali kiasi cha fedha zaidi ya Bilioni 12 kwenye ujenzi wake. (Picha na George Mwigulu) |
Ni sehemu ya Nyaya zitakazo tumika kuuganisha umeme katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambazo zimewasili leo Tarehe 07,January ,2023.
Ameeleza kwa Mwezi huu wa kwanza wanatalajia kupokea vifaa vyenye samani ya shilingi bilioni Tano ingawa hadi sasa wameshapokea vifaa mbalimbali vyenye samani ya shilingi Bilioni Moja kutoka Bohari ya Madawa [MSD] huku wakiendelea kusubilia vifaa mbalimbali kwaajili ya hospitali hiyo.
Mradi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Katavi kukamilika kwake na kuanza kutoa huduma ni faraja kwa wananchi wa mkoa wa Katavi kuepuka adha ya kufata Matibabu Makubwa katika mikoa ya Mbeya mwanaza na Tabora.