Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi,Beda Katani akizungumza ya kina na chombo hiki hivi karibuni- (Picha na Paul Mathias) |
Na George Mwigulu,Katavi.
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi,Beda Katani anajivunia mafanikio ya zaidi ya miaka 20 ya kukitumikia chama hicho kwa nyadhifa mbalimbali licha ya kutokuweza kuonekana kwenye duru nyingine ya uchanguzi wa ndani uliofanyika hivi karibuni.
Mwenekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi,Beda Katani akisisitiza jambo wakati wa mahojiano maalumu- (Picha na Paul Mathias) |
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi,Beda Katani anajivunia mafanikio ya zaidi ya miaka 20 ya kukitumikia chama hicho kwa nyadhifa mbalimbali licha ya kutokuweza kuonekana kwenye duru nyingine ya uchanguzi wa ndani uliofanyika hivi karibuni.
Akizungumza
na chombo hiki kwenye mahojiano maalumu katika viunga vya Garden Park Hotel Manispaa
ya Mpanda Mkoa wa Katavi anasema mafanikio yake sio ya kutiliwa shaka ndani ya
CCM,Serikalini nakwa wananchi wa hali chini.
Beda ameweka
wazi juhudi zake za kuwaunganisha wanachama na kuiamini serikali yao iliyoundwa
na CCM kuwa ndio kimbilio na mwarobani wa matatizo yao.
Anabainisha
kuwa wakati anaingia ndani ya uongozi ndani ya chama hicho hali haikuwa shwari
kutokana na baadhi ya maeneo kuwa ngome ya upinzani hali hiyo ilimpa hamasa ya
kufanya kazi kwa bidii ya kisiasa ili kukomboa maeneo hayo na kuwa chini ya CCM
kwa mfumo halali wa kidemokrasia unaotambuliwa na Katiba ya nchi “ Nilitumia
weledi na siasa safi kushawishi umma kukiamini chama Tawala”amebainisha.
Katika
kutatua matatizo ya wananchi alifungua milango muda wowote akiamini kwamba
suluhu ya matatizo ya wananchi yanakabiliwa kwa kuyatatua kwa vitendo.
CCM imekuwa
dira na mwongozo kwa watendaji wa serikali kwa kuhakikisha ilani ya chama inatekelezwa
na wakati mwingi ilimbidi kuwa mkali kukemea ubadirifu wa fedha za umma na
uzembe kwa masirahi ya wananchi bila kujali itikadi zao.
“…nakumbuka
nikiwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa nilitembelea Kata ya Mwamkuru na kubaini
msingi moja ya majengo ulikuwa umejengwa chini ya kiwango na nilitambua hivyo
baada ya kuomba jembe na kutindua na nilijionea kiwango kidogo zaidi cha
cementi kilichokuwa kimetumika kujengea” Amesema Beda.
Amesema Msitaafu huyo “Baada ya kitendo hicho wataalamu walikuja na kubaini kile nilichokiona mimi,na ndipo jina la Mhadisi nilipolipata kwa kuwa nao walijiridhisha kwa kubaini mapungufu hayohayo ambayo nami niliyabaini kwa macho na hisia zangu”.
Vilevile ameeleza kuwa uhodari wake wa kutafuta ufumbuzi kwenye masuala kadha wa kadha magumu ya wananchi kwa kuamini kuwa akitatua matatizo ya wananchi ndiyo salama ya Serikali na CCM.
“Kazi za
ufumbuzi wa matatizo zilinifanya niitwe Daktari” ameweka wazi hivyo.
Kuhusu
uwajibikaji kwa watendaji wa serikali
ndani ya uongozi wake inatajwa kuwa alikuwa mkali.
“…labda watu wananitafsri ukali wangu ulikuwa
katika sura ya kiutendaji kwa kuamini kuwa kazi ya chama ni kuisimamia serikali”amesema
hayo huku akieleza kuwa uongozi wake ulikiunganisha Chama na Serikali na
hapakuwa na uadui wowote dhidi ya watumishi wa serikali na chama.
“…kunakosa gani
la kumpigia simu kiongozi Mhandisi, au Meneja yeyote wa Taasisi ya umma kwa
lengo la kufahamu namna wanavyotatua shida za wanachi kupitia malalamiko ninayoyapata
kutoka kwa wananchi?.“ alihoji Beda”
Aidha anaamini ufumbuzi wa mataizo ya wananchi utaendelea kufanyika ndani ya uongozi mpya kwa kuwa CCM inawanachama imara na wenyewe uwenzo mkubwa wa kufanya kazi kwa masirahi mapana ya Chama na Taifa kwa ujumka huku akisema kuwa Chama amekiacha kikiwa na nguvu na kuaminiwa na wananchi.
Mwendelezo wa Makala hii itakuwa
wiki ijayo ambapo Mh Mwenyekiti Mstaafu CCM Mkoa wa Katavi,Beda Katani ataelezea
ni namna gani alivyopokea utenguzi wa zuio la mikutano ya hadhara na Mh Rais
Dkt Samia Suluhu Hassan.
Tufuate kwenye kusarasa zetu
Twitter/Instagram @katavipc na Facebook Katavi Press Club.