Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwa mkoani Katavi kwa ziara ya siku mbili - (Picha na Paul Mathias) |
Na George Mwigulu, Katavi
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewapongeza wanahabari wa Mkoa wa Katavi kwa kuendelea kuandika habari zinazoutangaza mkoa wa huo kwenye mambo mbalimbali.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akisalimiana na viongozi mbalimbali wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Katavi. (Picha na Paul Mathias) |
Amesema hayo leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Katavi,Mwamvua Mrindoko baada ya kusomewa
taarifa ya mkoa akiwa kwenye ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani hapa.
Nape ameeleza kuwa amekuwa akizisikia habari za
Mkoa wa Katavi kupitia vyombo vya habari
vikielezea masuala mbalimbali.
“niwapongeze wanahabari wa Katavi tunazisikia
habari za Katavi…RAS anasema hawapo wabobezi lakini wabobezi wanatengezwa
taratibu na mimi naamini katika kazi hiyo hiyo mnayoifanya basi tutapata wabobezi wa kutosha” Amesema Nape.
Aidha amesisitiza kuwa wizara hiyo itaendelea kuhamasisha watu kuja kuwekeza wenye sekta ya mawasiliano na habari kwa kuwa mkoa wa Katavi unakua kwa kasi na kuwa na mabadiliko makubwa.
Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi (waliosimama) wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kazi- (Picha na Paul Mathias) |
Vilevile kwa upande waandishi wa habari wa Mkoa
wa Katavi wakisema kwa masharti ya kutokutajwa jina lake ameeleza kuwa viongozi
wa Mkoa wa huo watambue umuhimu wa waandishi wa habari kwa kuwa kiungo cha
utendaji kazi baina yao na wananchi
wanaowatumikia.
Ameeleza kuwa kitendo cha Waziri wa Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuwapongeza waanahabari
hadhari mbele ya viongozi mbalimbali wa mkoa ni ishara njema ya kuacha somo
ambalo kama litafanyiwa kazi litaweza kukuza tanisia ya habari.
Alex Ngereza Mwandishi wa habari wa Radio Free
Africa na Start Tv wa Mkoa wa Katavi ameishukuru serikali kupitia waziri Nape
kwa kuona mchango wa waandishi wa habari akishauri kuwa kama wizara husika
imeona juhudi za kuhabarisha umma zinazofanywa na kundi hilo.
Amefafanua kila kuna haja ya serikali ya mkoa wa Katavi kuangalia namna bora ya kuweka mazingira wezeshi ya kuwainua kiuchumi kupitia kazi wanazozifanya.