Na Walter Mguluchuma-Katavi
Waziri wa Mawasiliano na Tekinojia ya Habari Nape Nauye amewataka Tanzania kutumia vizuri mawasiliano kwa kuweza kujiajiri na wasitumie mawasiliano kwa kutapeli watu bali watumie kwa kujiletea maendeleo .
Waziri wa Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari Nape Nauye amewataka wa Tanzania kutumia vizuri mawasiliano kwa kuweza kujiajiri na wasitumie mawasiliano kwa kutapeli watu bali watumie kwa kujiletea maendeleo
Wito huu ameutowa Wilayani Mlele Mkoani Katavi wakati alipokuwa akizindua mnara wa mawasiliano uliojengwa na TTCL kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano kwa wote.
Amesema
watanzania watumie uwepo wa mawasiliano kwa kujipatia ajira na kwa
ajiri ya maendeleo na wasitumie vibaya
kwa kutapeli kudanganya watu na kudanganya watoto wadogo wa kike wanafunzi .
Nape amebainisha kuwa tutumie uwepo wa masiliano kwa vijana kuweza kujiajiri na tusitumie kwa umbea tutumie kwa ajiri ya maendeleo ya kilimo na katika biashara mbambali zitakazo weza kutupatia fedha .
Amesema miradi hiyo ya minara imejengwa kwa
fedha za walipa kodi wananchi hivyo ni mali ya wananchi wenyewe hivyo wailinde ,waitunze waisimamie ni rahisi kuzani kwa kuwa
imejengwa na TTCL na mamlaka ya mawasiliano na kudhani kuwa si mali ya
wananchi , wao kazi yao kama Serikali ni
kuiliendelea kuihudumia waitunze
hivyo wananchi wailinde.
Waziri wa Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari Nape Nauye akitoa neno baada ya kuzindua mnara wa TTCL Katika halmashauri ya Mlele Mkoa wa Katavi [picha na paul mathias] |
Mkurugenzi Mkuu waMfuko wa Mawasiliano kwa wote Justina Mashiba amesema mamlaka hiyo inatekeleza shughuli zake kwa kuwa na miradi Nchi nzima kwenye kila Wilaya ya na Mkoa .
Mashiba amebainisha kuwa hadi sasa wameisha kushirikiana na watowa huduma mbambali wa mawasiliano kama TTCL , Tigo Voda com,Airtel na Makampuni mengine wameisha saini mikataba ya ujenzi wa minara 1242 ya mawasiliano kwa nchi nzima na kati ya minara hiyo minara 1087 imeisha kamilika .
Amesema
minara ambayo iliyobakia kujengwa ni 155 ambayo nayo ipo kwenye hatua mbambali
za ukamilishwaji na itakapokuwa imekamilika itakuwa minara 1242 watakuwa wamewafikia Wanzania milioni
15.
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Peter Ulanga amesema TTCL inaendelea kuboresha mawasiliano kwenye maeneo yote ambayo hayana mawasiliano yakiwepo maeneo ya mikoa ya pembezoni.