WALANGUZI WA TUMBAKU KATAVI KUKIONA CHA MTEMA KUNI


Mkuu wa mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiwa hutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa 29 wa Mwaka wa chama kikuu cha ushirika Latcu katika mkoa wa Katavi. [Picha na Paul mathias]
 
Na Paul Mathias -Katavi
Wakulima wa zao la Tumbaku katika mkoa wa katavi wameaswa kutouza zao la Tumbaku Kwa walanguzi binafsi kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea vyama vya ushirika Kuingia katika Matatizo ya kujiendesha.


Mkuu wa mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko[ wanne kutoka kushoto walio kaa] kulia kwake Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika Latcu, Dorashazi Venasi pamoja na wabunge kutoka mkoa wa katavi  wakwanza kushoto alie kaa Anna  Lupembe Mbunge wa jimbo la nsimbo na wapili nawapili toka kulia aliekaa Sulemani Moshi kakoso mbunge wa Mpanda vijijini [picha na Paul Mathias]

Wakulima wa zao la Tumbaku katika mkoa wa katavi wameaswa kutouza zao la Tumbaku Kwa walanguzi binafsi kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea vyama vya ushirika Kuingia katika Matatizo ya kujiendesha.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko wakati akiuhutubia Wajumbe wa mkutano Mkuu wa 29 wa mwaka wa chama kikuu Cha ushirika Latcu katika mkoa wa katavi uliofanyika katika Ukumbi wa Katavi resort Mpanda Mjini. 

 Mrindoko amesema kulikuwa na matatizo makubwa kwenye Vyama vya Msingi kutokana na baadhi ya wakulima kuuza Tumbaku zao Kwa watu binafsi kitendo ambacho nikinyume na miongozo ya ununuzi wa zao Hilo .

 Amefafanua kuwa Mkoa wa katavi hauko tayari kuona unaingia katika shida hiyo Kwa baadhi ya watu wasiokuwa waadilifu Kwa kujipenyeza Kwa wakulima na Kununua Tumbaku kinyume na Sheria nukuu.

”tumekuwa tukipata changamoto katika misimu mbalimbali mfano kwenye zao la Tumbaku wapo wakulima Binafsi wanajihusisha na ununuzi na uuzaji wa Tumbaku swala hili ni Malufuku kwa mujibu wa sheria nitoe maelekezo hapa kwamba hatutamvumilia mtubinafsi ambae atajihusisha na ununuzi wa Tumbaku kwa mtu binafsi sheria za ununuzi wa Tumbaku zipo wazi amesisita Mrindoko''

Baadhi ya Wajumbe wakiwa katika Mkutano mkuu wa 29 wa chama kikuu cha ushirika latcu kilichofanyika katika ukumbi wa Katavi Resort Mpanda Mjini.
Aidha katika hatua nyingine ametoa siku 14 Kwa Kwa Kampuni ya ununuzi wa Pamba ya NGS kuhakikisha wanalipa ushuru wa mazao Kwa halmashauri na Vyama Msingi kama takwa lakisheria linavyosema Ili ziweze kutenda kazi Kwa weledi Kwa wakulima na wananchi Kwa ujumla

Amesema mazao ya Tumbaku na Pamba yamekuwa yakichangia pakubwa mapatoya  Mkoa  kupitia halmashauri ndiyo maana serikali ya Mkoa imekuwa ikiendelea kuvisimamia Vyama hivi Kwa ukaribu ukiwa ni sehemu ya kuhakikisha ufanisi kiutendaji unakuepo.
 
Kuhusu Makampuni ya ununuzi wa Tumbaku amesema Makampuni hayo yafanyekazi Kwa mujibu wa taratibu zinavyoelekeza Kwa kuzingatia masilahi mapana ya wakulima Ili waweze kujikwamua kutoka sehemu Moja na nyingine kiuchumi .

Mrajinsi msaiidizi Mkoa wa katavi Peter Nyakunga amebainisha kuwa atahakikisha Vyama vya Msingi katika mkoa wa katavi vinaendelea kustawi Kwa kuvisimia kadri ya matakwa ya serikali Ili viendelee kuwa sehemu ya kukuza uchumi wa mkulima na pato la mkoa. Nyakunga ameeleza Kwa msimu huu wamejipanga vyema kuhakikisha Vyama vyote 20 vilivyolima Tumbaku watavisimamia katika hatua zote kuanzia hatua ya kulima Hadi kuvuna pasipokuwa na shida yeyote.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Sulemani Moshi kakoso akitoa salamu kwenye mkutano huo ametoa angalizo Kwa viongozi wa Vyama vya Msingi kufanya Kazi zao Kwa kuzingatia uadirifu Ili wakulima waweze kuwa na imani nao Kwa dhamana waliyopewa na wakulima. 

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijiji Selemani Moshi Kakoso akitoa neno katika mkutano mkuu wa 29 wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Katavi[ Picha na Paul mathias]
Kakoso amesisitiza  mara kadhaa kumekuwa na changamoto ya Migogoro kwenye Vyama vya Msingi inayosabishwa na baadhi ya viongozi wa Vyama hivyo ambao baadhi yao wamekuwa wakijisahau kuwa wao ndio kioo na Dira Kwa Vyama hivyo.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu huo akiwemo Iddy Ramadhani kutoka chama Cha Msingi Cha Ilunde Amcos amesema  ulanguzi wa Tumbaku imekuwa changamoto kutokana na baadhi ya wakulima kutokuwa na fedha hasa nyakati za msimu wa kilimo Hali ambayo huingia katika wimbi la ulaghai na walanguzi wa Tumbaku ambao sio rasmi.

Amesema Ili kuthibiti Hali hiyo lazima kufanyike Makakati madhubuti Ili kuhakikisha mkulima Kwa wakati huo wa uhitaji wa fedha awe na uwezeshwaji kupitia mfumo Rasmi Kwa mazingira yanayowekana Kwa kushirikiana na Serikali.

 Mkutano Mkuu wa 29 wa mwaka wa chama kikuuu Cha wakulima Latcu Kimehudhuliwa na wajumbe mbalimbali wa Vyama vya Msingi wanunuzi wa Tumbaku, Taassi za fedha,na Viongozi wa Vyama vya Msingi kiuwakilishi kutoka mikoa ya Tabora,Mbeya,na Kigoma.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages