WAZIRI NAPE ALIFANYIA KAZI OMBI LA WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA.

Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,Nape Nnauye.

George Mwigulu na Paul Mathias

Serikali kupitia Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeadhamilia kwa muda wa miezi minne hadi sita ijayo kuimarisha huduma ya mawasiliano na TEHAMA ndani ya chuo cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda,Halmashuri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizumzia masuala mbalimbali ya mkoa wa Katavi kwenye sekta ya mawasiliano na Habari.

Serikali kupitia Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeadhamilia kwa muda wa miezi minne hadi sita ijayo kuimarisha huduma ya mawasiliano na TEHAMA ndani ya chuo cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda,Halmashuri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi.

Waziri wa Wizara hiyo Nape Nnauye amesema hayo  leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiwa kwenye ziara yake ya siku mbili ya kikazi ambapo ameleza lengo la ziara anazozifanya katika mikao ya mipakani na pembezoni ni kungalia hali ya mawasiliano na huduma za habari hasa zinatolewa na shirika la utangazaji la taifa (TBC) kama sehemu utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mikoa ya pembezoni na hasa mipakani mawasiliano yanaimarishwa ili kuchochea ukuaji wa lugha ya Kiswahili na tamaduni zetu kwenye nchi jirani.

Nnauye ameeleza kuwa alielezwa siku za nyuma na Waziri Mkuu Mstafuu,Mizengo Pinda pale Kibaoni katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Kampasi ya Mizengo Pinda kunachangamoto ya huduma ya mawasiliano na katika kipindi hiki cha TEHAMA wanahitaji wakati mwingine kufundishwa wakiwa palepale na walimu kutoka SUA kwa mfumo wa TEHEMA.

“Nimepita hapo ili kutatua changamoto hiyo na tumekubaliana kuanzia mwenzi huu makampuni kama VODACOM watakwenda kuongeza uwezo wa mnara kutoka 2G hadi 4G ili uongeze nguvu huku TTCL watachukua mkongo wa mawasiliano ya taifa kutoka Kizi kuupeleka pale chuoni ili kusaidie huduma za mawasiliano chuoni hapo na maeneo jirani” amesema Nnauye

Waziri huyo amesema kuwa serikali kupitia wizara yake inamiradi ya kuimarisha mawasiliano mipakani kwani ndani ya mipaka hiyo kuna shughuri nyingi  za kibishara zinafanyika na kutowauganisha kwenye huduma za mawasiliano ni kutokuwasaidia kibiashara na kuikosesha serikali mapato.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa kwa nchi nzima kuna miradi ya minara 763 mipya itakayojengwa ambayo tenda yake imetangazwa ambapo Mkoa wa Katavi itakuwa sehemu ya wananufaika wa minara hiyo.

Aidha amesema “…Tunao mradi  kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote utakao wezesha minara 488 kuongezewa uwezo na kwa Mkoa wa Katavi kuna minara 14 inaongezwa uwezo wake hii ni kwasababu minara mingi ilipojengwa kwa mara ya kwanza ilijengwa kwa uwezo wa kuhudumia vitochi zaidi kwa ajili ya kupiga simu.Sasa tunaiongezea uwezo minara kutoa huduma hasa za data”

Baadhi ya viongozi wa kamati ya ulizi na usalama ya Mkoa wa Katavi wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa ziara ya waziri Nape Nnauye.

Vilevile Nnauye katika kuhakikisha mradi wa ujenzi wa minara mpya unafanyika kwa kasi amemwomba Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko kuwasaidia maeneo ya ujengwaji wa minara hasa maeneo ya vijijini ambapo uzoefu uonesha kumekuwa na chagamoto ya upatikana.

Upatikanaji wa vibali vya watu wa mazingira wakati mwingine inatukwamisha kwani ujenzi wa minara  unatuonesha inajengwa kwa mienzi 2 hadi 3 lakini tunajenga kwa mienzi 9 kwa sababu mienzi karibia 6 niyakutafuta vibali …mkiwasukuma watoa vibali watajenga kwa wakati na wananchi kuanza kupata huduma ya mawasiliano” amesisitiza Waziri Nnauye.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko amemwomba Waziri huyo kuweka miundombinu ya mawasiliano katika barabara iendayo Mkoa wa Tabora hasa katika maeneo ya Nsimbo hadi Inyonga na Inyoga hadi Ipole.

Ameeleza kuwa kuimarishwa kwa mawasiliano ya maeneo hayo yataimarisha zaidi usalama kwa abiria wanaosafiri kwa mabus yaendayo mikoa mingine.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa ngazi ya mkoa wa Katavi wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Awali akisoma taarifa mbele ya Waziri Nnauye,Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,Abbas Rugwa hali ya huduma ya mawasiliano na habari niyakuridhisha ingawa kuna baadhi ya maeneo hasa ya vijijini hayajafikiwa.

Katibu Tawala huyo amesema kuwa ongezeko la idadi ya watu kutoka laki tano hadi zaidi ya milioni moja ni ishara ya kuaji wa mkoa ambao unapaswa kwenda sambamba na uwekezaji zaidi kwenye huduma ya mawasiliano na habari.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages